Naomba ushauri kuhusu uagizaji magari kutoa Japan au Afrika Kusini

meruly

Member
Joined
Mar 2, 2024
Posts
56
Reaction score
50
Habari wadau!

Mimi ni transport Manager wa shule moja hapa nchini,tunahitaji Magari mengi madogo na makwa kwajili ya kubeba wanafunzi.

Swali langu kati ya hizi nchi mbili wapi nitapata Magari yenye ubora kwa bei rahisi?

1. South Africa
2. Japan

KUHUSU MAKAMPUNI YA UGAIZAJI.
Tunataka hii kazi tuwape Makampuni ya wazawa hapa nchi ambayo yana connection za uagizaji,ni kampunigani the best tuwape kazi?

1. Yakwetu motors
2. Digxam
3. AV Magari
 
Habari wadau!
Mimi ni transport Manager wa shule moja hapa nchini,tunahitaji Magari mengi madogo na makwa kwajili ya kubeba wanafunzi,

Swali langu kati ya hizi nchi mbili wapi nitapata Magari yenye ubora kwa bei rahisi?
1.South Africa
2.Japan

KUHUSU MAKAMPUNI YA UGAIZAJI.
Tunataka hii kazi tuwape Makampuni ya wazawa hapa nchi ambayo yana connection za uagizaji,ni kampunigani the best tuwape kazi?

1.Yakwetu motors
2.Digxam
3.AV Magari
Hii tenda ungewapa wana JF wenzako ingependeza.
 
Habari wadau!

Mimi ni transport Manager wa shule moja hapa nchini,tunahitaji Magari mengi madogo na makwa kwajili ya kubeba wanafunzi.

Swali langu kati ya hizi nchi mbili wapi nitapata Magari yenye ubora kwa bei rahisi?

1. South Africa
2. Japan

KUHUSU MAKAMPUNI YA UGAIZAJI.
Tunataka hii kazi tuwape Makampuni ya wazawa hapa nchi ambayo yana connection za uagizaji,ni kampunigani the best tuwape kazi?

1. Yakwetu motors
2. Digxam
3. AV Magari
Wewe Kama mfanya biashara nilitegemea kigezo Kikubwa kiwe value for money. Sasa hapa naona issues za uzawa! Good luck!
 
Unapataje value ya pesa bila kuinua wazawa ambao wametuinua hadi shule ikafika hapa ilipo,nimepita kwenye kampuni za uuzaji wa Magari wengi ni wageni,unashauri niangali value ya pesa kwakuwainu wageni na kuwaacha wazawa ambao wametuinua sisi au?
 
TUNAHITAJI TOYOTA COASTER 5
NISSAN CIVILIAN 3
TOYOTA HIACE 2
NISSAN CALAVAN 3

Bei gani @ GARI?
 
TUNAHITAJI TOYOTA COASTER 5
NISSAN CIVILIAN 3
TOYOTA HIACE 2
NISSAN CALAVAN 3

Bei gani @ GARI?
Hapo Chukua Toyota Coaster zenye engine ya 14B kama mtakuwa na safari ndefu au tour na wanafunzi Coaster 2 nunueni zenye engine ya 1hd fte, NO4C.

Msichanganye brand Toyota na Nissan, ukiwa na brand moja ni rahisi kumanage fleet ya gari zako kuanzia kununua spare,ufundi na running cost.

Nissan Civilian bei saizi inalingana na Toyota Coaster, Nissan Civilian W41 (mayai) kama utachukua kwa shunting za kubeba watoto chukua yenye engine ya Zd30 au Td42, engine ya 4m51 achana nayo haitokuwa rafiki kwa kazi zako. Kama utakuwa na madereva wazuri na mafundi makini ukipata Zd30 engine hii itakuwa faida kwako ina fuel consumption nzuri sana.
 
TUNAHITAJI TOYOTA COASTER 5
NISSAN CIVILIAN 3
TOYOTA HIACE 2
NISSAN CALAVAN 3

Bei gani @ GARI?
Kwa South Africa hakuna Toyota Coaster na Nissan Civilian.

South Africa utapata Toyota Hiace Quantum za kuanzia 2010 kuja juuzinakuja na engine za petrol (1TR,2TR,3RZ) na diesel (1Kd,2kd,1gd,2gd).Bei yake inacheza kuanzia 40m na kuendelea kulingana na mwaka

Nissan Caravan, South Africa wao wanaita Nissan Nv300 (Impendulo) hizi nyingi zipo za diesel zenye engine ya zd30 na miaka ya karibuni wanatumia Engine ya Yd25 hii kama ya kwenye Nissan Hardbody na Navara. Bei nazo zinaanzia 35m
 
Asante South Africa naitoa kwenye hesabu.
 
Hapo Chukua Toyota Coaster zenye engine ya 14B kama mtakuwa na safari ndefu au tour na wanafunzi Coaster 2 nunueni zenye engine ya 1hd fte, NO4C.

Msichanganye brand Toyota na Nissan, ukiwa na brand moja ni rahisi kumanage fleet ya gari zako kuanzia kununua spare,ufundi na running cost.

Nissan Civilian bei saizi inalingana na Toyota Coaster, Nissan Civilian W41 (mayai) kama utachukua kwa shunting za kubeba watoto chukua yenye engine ya Zd30 au Td42, engine ya 4m51 achana nayo haitokuwa rafiki kwa kazi zako. Kama utakuwa na madereva wazuri na mafundi makini ukipata Zd30 engine hii itakuwa faida kwako ina fuel consumption nzuri sana.
Tumeisha kaa kikao nakupitisha haya Magri ningungu kuitisha tena kikao kingine kwajili ya kupangua maamuzi ya mwanzo.

Digxam walisema watatupatia Magari yenye Engine za 1HZ upande wa Coaster na Nissan Civilian Engine ya TD4.2 yatakuja na rangi na logo ya shule, Pia bei zinatofautiana kwakiasi kikubwa nikilinganisha na uchambuzi wako hapo juu ,pia wata delivery hadi Mzigo ufike Dar Bandarini kisha tukague nakulipa pesa yao vipi hizo Engine zinachangamoto gani kama unazijua?
 
sasa kumbe umeshafika hatua hiyo hapo si bado kubargain tu price ulipie
 
Tumeisha kaa kikao nakupitisha haya Magri ningungu kuitisha tena kikao kingine kwajili ya kupangua maamuzi ya mwanzo.

Digxam walisema watatupatia Magari yenye Engine za 1HZ upande wa Coaster na Nissan Civilian Engine ya TD4.2 yatakuja na rangi na logo ya shule, Pia bei zinatofautiana kwakiasi kikubwa nikilinganisha na uchambuzi wako hapo juu ,pia wata delivery hadi Mzigo ufike Dar Bandarini kisha tukague nakulipa pesa yao vipi hizo Engine zinachangamoto gani kama unazijua?
Sawa, mmeamua kuchanganya brand za Toyota na Nissan baada ya kukubaliana kwenye kikao.

Hii mmeweka ili mpime ufanisi na gharama za kuendesha kati ya Toyota Coaster na Nissan Civilian.
 
Tumeisha kaa kikao nakupitisha haya Magri ningungu kuitisha tena kikao kingine kwajili ya kupangua maamuzi ya mwanzo.

Digxam walisema watatupatia Magari yenye Engine za 1HZ upande wa Coaster na Nissan Civilian Engine ya TD4.2 yatakuja na rangi na logo ya shule, Pia bei zinatofautiana kwakiasi kikubwa nikilinganisha na uchambuzi wako hapo juu ,pia wata delivery hadi Mzigo ufike Dar Bandarini kisha tukague nakulipa pesa yao vipi hizo Engine zinachangamoto gani kama unazijua?
Huyo Supplier wenu katumia kigezo kipi cha kuwapa Coaster yenye Engine ya 1hz. Wakati nyie hamuendi kufanya heavy duty trips. Kazi yenu ya kubeba wanafunzi Engine za 13B na 14B zingewafaa zaidi sababu zipo economy kuzidi 1hz na Running Cost ni ndogo.

Civilian anawapa Td42 wakati kuna mbadala wa Zd30 yenye utumiaji mzuri wa mafuta ipo kwenye Nissan Civilian W41.

Engine zote alizowachagulia hazina changamoto ni Engine stamilivu kwenye hali nzuri na ngumu.

Coaster(B50) na Civilian(W41) inabidi mchukue za kuanzia mwaka 2000 kuja juu na mumpe supplier condition ziwe Long Base( gari ndefu) ili muwe na faida ya kubeba wanafunzi wengi. Hizo basi zipo fupi (Short Base) na ndefu (Long Base) hata uwezo wa kubeba abiria ni tofauti.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Back
Top Bottom