Nimewahi kufunga system za umwagiliaji kwenye greenhouse za mboga na maua. Ukubwa wa kila greenhouse moja ni wastani wa nusu ekari, na kila greenhouse mbili zilikuwa zinashea tank tower moja yenye tank ya 5000L capacity (Yale marefu yenye kitako chembamba na sio mapana yenye kitako kikubwa). Ingawa technology iliyotumika ni drip irrigation. Kinachofanyika , ili kuongeza pressure huwa tunapunguza size ya bomba, otherwise uwe unatumia surface irrigation.
Kwa ekari 4 unaweza Jenga minara miwili tu ya kubeba Lita 5000L kila moja, na kila ekari 2 zikashea tank moja. Kinachofanyika ni kumwagilia kwa shift. Let say, saa 3 mpaka saa 5 tank A linamwagilia shamba No.1 na tank B linamwagilia shamba No.3. saa 5 mpaka saa 7 tank A linamwagilia shamba No. 2 na tank B kumwagilia shamba No. 4. Just simple Sana ndugu, ni kiasi cha kuweka gate valve zako vizuri according to shamba plan yako na topography ya shamba lako tu.
Kuhusu kupandisha maji, pump yako itatoa maji kutoka underground/source up to the tank, ndio maana binafsi nikashauri pump iwe yenye head kubwa na discharge kubwa kulingana na tank zako. Kuliko kununua pump mbili, issue ya initial cost, operation costs na maintenance costs lazima ziwe juu.
Zaidi hebu tusubiri na wadau wengine waje watupe mawazo na ushauri/uzoefu zaidi. Usisahau kuwa, Kama source ni kisima cha maji chumvi, surface irrigation ni harmful kwa uhai wa shamba lako pia.