Naomba Ushauri: Kununua na kutumia line za Tigopesa na M-Pesa kutoka kwa wakala aliyezitumia

Babu Kijana

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2013
Posts
587
Reaction score
276
Habari za leo mabibi na mabwana,

Nina mpango wa kununua line za Tigopesa na M-Pesa kutoka kwa wakala ambae ameacha kufanya biashara hiyo ya uwakala na kuamua kuziuza line zake. Kama mnavyojua kuanzisha uwakala kutoka kwa wakala mkuu ni shilingi milioni moja kwa kila line na mimi siwezi kuzimudu gharama hizo kwa sasa, njia pekee ni kununua kwa mtu kwa gharama ya chini na kujiendelezea mtaji binafsi.

Ushauri ninaotaka kutoka kwenu je ni njia salama kununua kwa mtu na tahadhari zipi nizichukue
​? na je nihakikishe vitu gani au documents zozote ambazo natakiwa nikabidhiwe na huyo mtu anaeniuzia? Kama kuna yeyote anayeweza kunisaidia kupata uwakala wangu wa moja kwa moja kutoka kwa wakala mkuu au kampuni hizi za simu kwa bei nafuu chini ya m1 tafadhali anisaidie.

Nawasilisha.
 
Siku hiziline ni bure kabisa huna haja ya kununua andaa tin lesen na kitambulisho chako nenda kwa wakala mkubwa unapewa.madhara ya kununua line kwa mtu kukitokea wizi mhusika aliyekuuzia ndiye anayetambulika huwezi lipwa wala rudishiwa line kama siyo mhusika. Nenda makumbusho tigo, voda mlimani city na airtel morrocco umemaliza kazi.
 
Mkuu asante sana lakini unavyosema bure yani ni bure kabisaaa au kuna gharama yoyote?
 
Unatengenezewa bure baada ya hapo unaanza kweka float yako ambapo siku hizi hawana limit ila ili iweze kukulipa vizuri hakikisha kila line ina angalao laki tano na cash uwe na kama 1.5 mil utapata commission nzuri kwa ujumla mtaji kama mil 2 ukiwa sehemu nzuri yenye miamala mingi hukosi laki 6
 
Ahsante sana kaka mungu akubariki, nafikiri ngoja nijiandae j3 niwafuate huko
 
Unatengenezewa bure baada ya hapo unaanza kweka float yako ambapo siku hizi hawana limit ila ili iweze kukulipa vizuri hakikisha kila line ina angalao laki tano na cash uwe na kama 1.5 mil utapata commission nzuri kwa ujumla mtaji kama mil 2 ukiwa sehemu nzuri yenye miamala mingi hukosi laki 6
Mkuu umefanunua vizuri tu,naomba unijuze kwa Airtel nikianza na 1mil Comission yao nitapata sh ngapi?
 
Siku hiziline ni bure kabisa huna haja ya kununua andaa tin lesen na kitambulisho chako nenda kwa wakala mkubwa unapewa.madhara ya kununua line kwa mtu kukitokea wizi mhusika aliyekuuzia ndiye anayetambulika huwezi lipwa wala rudishiwa line kama siyo mhusika. Nenda makumbusho tigo, voda mlimani city na airtel morrocco umemaliza kazi.

Mkuu hiyo tini lesen unaipata wapi na yenyewe ni hela au nayo bure?
 
Nahitaji line ya M PESA NA AIRTEL MONEY ARUSHA mwenye kuweza kunipatia tafadhali.
 
Back
Top Bottom