Babu Kijana
JF-Expert Member
- Jan 24, 2013
- 587
- 276
Habari za leo mabibi na mabwana,
Nina mpango wa kununua line za Tigopesa na M-Pesa kutoka kwa wakala ambae ameacha kufanya biashara hiyo ya uwakala na kuamua kuziuza line zake. Kama mnavyojua kuanzisha uwakala kutoka kwa wakala mkuu ni shilingi milioni moja kwa kila line na mimi siwezi kuzimudu gharama hizo kwa sasa, njia pekee ni kununua kwa mtu kwa gharama ya chini na kujiendelezea mtaji binafsi.
Ushauri ninaotaka kutoka kwenu je ni njia salama kununua kwa mtu na tahadhari zipi nizichukue​? na je nihakikishe vitu gani au documents zozote ambazo natakiwa nikabidhiwe na huyo mtu anaeniuzia? Kama kuna yeyote anayeweza kunisaidia kupata uwakala wangu wa moja kwa moja kutoka kwa wakala mkuu au kampuni hizi za simu kwa bei nafuu chini ya m1 tafadhali anisaidie.
Nawasilisha.