Naomba ushauri kwa ramani hii

Naomba ushauri kwa ramani hii

Goguryeo

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2019
Posts
3,003
Reaction score
5,653
Wakuu,

Ni matumaini yangu mpo bukhery.

Naombeni msaada wenu hapa kwenye haka karamani.

Target yangu ilikua ni kutumia tofali range ya 3200-3600 ....

Sasa nimeambiwa tofali 4300 kichwa kinawaka moto.

Msaada wenu wakuu.
 
Kuna kenge alinichorea ramani akaniambia nyumba nzima niliyokuwa naitaka kuanzia msingi hadi kukamilika ni tofauti 1000 nikaona kujenga kumbe rahisi sana,picha linaanza msingi pekee tofauti 700,zikakatika nitakuja kumpiga makofi yule chizi
 
Ramani mbovu, manafasi makubwa halafu haina stoo. zipo za vyumba kama hivuo za tofari ulizonazo. ila kama umeipenda hiyo ongeza tofari
 
Nyumba sio ndogo, ina passages nyingi na kona za kutosha. Tofali 4,500 kawaida sana. Tena kama unajenga kwenye sloped area zaweza kuongezeka.

Hata hivyo, kwenye ujenzi tofali sio za kuwazia sana.
 
Wakuu,

Ni matumaini yangu mpo bukhery.

Naombeni msaada wenu hapa kwenye haka karamani.

Target yangu ilikua ni kutumia tofali range ya 3200-3600 ....

Sasa nimeambiwa tofali 4300 kichwa kinawaka moto.

Msaada wenu wakuu.

View attachment 2678706
Binafsi, sipendi public washroom iwe na choo na bafu kwenye kichumba kimoja. Mtu akiwa anaharisha na anataka kuingia chooni na wakati huo huo mwingine yupo bafuni anaoga, huyu wa kuharisha atajiharishia. Tafuta namna utenganishe hizi sehemu mbili.
 
Nyumba ina almost 182m² unadhani ni ndogo hii?

Tofali 4,500+
Cement 200+
Kokoto 15m³
Mchanga 40m³
.....
 
Wakati wa kuvaa na kupaka make ups lazima uwe na tochi😂😂😂
Korido nyingi zisizo na maana
 
Siku hizi sebule kubwa ni mateso,kuanzia kwenye kununua mapazia,masofa n.k
Punguza ukubwa wa sebule,stoo na master bedroom-hicho chumba cha dressing cha nini??
Ondoa makorido yanachukua space na kuongeza ukubwa wa nyumba.
Tengeneza ramani inayoendana na uchumi wako,aftr law nyumba zenyewe wanaume ukiishi sana miaka 15.
 
Humu ndani ukikaa vibaya utajihisi masikini peke yako. Sasa wewe umeshindwa kumshirikisha mkeo au mkandarasi wako kweli Hadi uje kutusumbua hapa? Ngoja tupambane na Bandar Kwanza mkuu
 
Siku hizi sebule kubwa ni mateso,kuanzia kwenye kununua mapazia,masofa n.k
Punguza ukubwa wa sebule,stoo na master bedroom-hicho chumba cha dressing cha nini??
Ondoa makorido yanachukua space na kuongeza ukubwa wa nyumba.
Tengeneza ramani inayoendana na uchumi wako,aftr law nyumba zenyewe wanaume ukiishi sana miaka 15.
Sebule kuwa spacious sio shida, ahida ni hizo corridor, zinachukua spaces bila sababu. Siku hizi designs za kutosha zipo ambazo hakuna makorido mengi. Standard house yenye 150m² kwa uchumi wa kawaida.
 
Back
Top Bottom