Habari wanaJF
Nakuja kweni naomba ushauri wa gari aina ya Mistubishi Pajero Mini.
1.Upatikanaji wa 'spare'
2.Matatizo ya hizi gari
3.ushauri wa bandari bila kuhusisha kodi ya TRA
MITSUBISHI PAJERO MIN XR II
(FIRST GENERETION)
MITSUBISHI PAJERO MIN XR II hii ni gari ndogo ambayo ina umbo lenye milango 3 huku ikiwa na cc 659 injininyake ikitoa power ya 59Nm na Tarqure ni 44 huku ikiwa na 5 speed .
MITSUBISHI PAJERO MIN inazo zaidi ya generetion tatu mpk sasa mm sitaki kuzielezea generetion nyingine na usiniulize ukinitaka nifate in box mwanga kwacha nitakuelezea ...leo ninaelezea tu kizazi cha kwanza cha
MITSUBISHI PAJERO MIN ambacho kilianza mwaka 1994-1998 hayo matoleo mengine nitafute praivet ukiwa na swadaka
Hiii ni moja kati ya gari ngumu sana na ni gari inayofaa sana kwenda nayo pori kwa sababu muda wote ina 4WD ,kukufanya mahalai popote kupita nayo bila ya kuwa na shoda yoyote hii iliundwa kwa ajili ya off road yaani barabara ya vumbi na tope kizazi cha kwanza cha gari hii kilijulikana kama( E51-E56) suv
Katika uchambuzi wa leo tutaangalia zaidi toleo la mwaka 1996 gari hili lilikuwa na uzito kg 780 gari hili kulingana cc zake kuwa ndogo lilikuja na injini ya 4A30 ambayo ilikuwa. Na top speed ya 129 km/h hivyo kwa mwendo liko tarataibu sana slow but sure
Upande wa matumizi ya mafuta kiukweli pajero mini walichemka sana labda kwa kuwa ni toleo la kwanza lilikuwa mwanzo huwa mgumu
[emoji91][emoji91]Injini ya cc 659 inatumia km 16 kwa lita 1 bila kuwasha Ac
[emoji91][emoji91]Ukiwasha kiyoyozi inatumia km 14 kwa lita 1
Upande wa acceleration
Inatoka 0-100km kwa sekunde 18.9
Hivyo mm nasema kuwa injini yake ni nzito sana kwenye kuchanganya ndio maaana nilisema ni slow but sure
Transmition ya gari hili ni manual
Upande wa ground clearence
Hapa wamejitahidi sana kutokana na kulitengeneza kuwa la kwendea pori lipo juu uvungu wake una 6.8 inch hivyo popote pale unaweza kwenda nalo bila ya kutokuwa na wac wàç wowote maana lina 4Wd muda wote halina 2WD
Uzuri wa gari hili ni
[emoji123]Ni gumu sana chuma cha pua
[emoji123]Kwa ndani nafasi yake ni kubwa
[emoji123]Linafaa sana mazingira ya pori sana mjini utakuwa unalionea
Ubaya wa gari hili
[emoji24]Nafasi kati ya viti vya nyuma ni ndogo
[emoji24]Lina mwendo kama wakobe yaani kwa mm hapana
[emoji24]Kwenye stering ni gumu sana linahitaji nguvu
[emoji24]Kwa wanawake kuliendesha hili linahitaji nguvu na kumbuka ni manual
Udhaifu wa gari hili
Hapa ndio sikuwahi kufikiria kabisa mpk mwalimu wangu wakijerumani pale chuo Passau - bavaria germany alituuliza swali katika MITSUBISHI PAJERO MIN REVIEW mnaliona liko sawa wote tulijibu ndio ,akasema mnakosea sanà
Ufafanuzi uko hivi
*Katika uundaji na kuchora mchoro wa gari hili EGENEER wa kijapani kuna kosa walilifanya ila waligundua muda umeenda swalinla kujiuliza
1.kwa nn gari kama hili lina cc ndogo linatumia mafuta mengi ? Linazidiwà hata na toyota tercel 1330 cc 4EFE
Jibu
Kuna makosa ya muundo. Wa injini 4A30 inatumia old electro caburetor ikiwa na single over head cam shaft drive chain hivyo kuifanya injini kuwa na mzigo mkubwa7500rm inatoa injini kuwa na mzunguko mkubwa na hivyo kupelekea ufanisi mdogo kwenye mafuta
2.bodi la gari lilisanifiwa vibaya watu waliosoma uhandisi wa magari watakubaliana na mm ,muundo wa gari hilinunasababisha ukinzani mkubwa gari lilikiwa kwenye mwendo hivyo kuiongezea injini uzito
3.kuliwekea muda wote 4WD wakati injini ina cc ndogo hili pia ni kosa walifanya wanaperekea injini kutumia mafuta mengi
[emoji177][emoji177]Ufanye nn kama una gari hili lisitumie mafuta mengi [emoji177][emoji177][emoji177]
1.punguza matumizi ya A.C ukiwa unaliendesha
2.tumia mafuta ambayo ni unleaded petrol yanapatikana kampuni chache tu za sheli hapa tz kama Puma ,Total ,Bp n.k hii itasaidia kuiongezea ufanisi injini yako na kufanya valve kuwa safi muda wote na injini itadumu sana
Mwisho
MITSUBISHI PAJERO MIN first generetion hiii ni gari ngumu sana , na inavilia mikiki yote kadri generetion zilivyokuwa zikibadilika na ndio pia na umbo lake lilikuwa linabdirika pia
Wajuzi wa mambo karibuni kwa nyongeza [emoji120] pamoja na mafundi mnauelewa mkubwa kuliko mm njooo mtoe nyongeza zenu