Naomba ushauri: Mpangaji wangu msumbufu kulipa kodi nataka nifungie vitu vyake

Usimfanyie hivyo, mpe muda andikishiana nae kwa mjumbe kwamba hadi kufikia let say Disemba mosi ulipe pesa yangu laa nitafunga chumba na nitazuia vitu vyako hadi hapo utakapokuja kulipa pesa yangu.
Ngojea nijaribu kufanya hivyo boss,japo nipo mbali nae,hofu yangu hasije kuhama usiku
 
Nikweli,inabidi niendenae taratibu tu, ngojea nimuandikie NOTICE kwamba Hadi muda fulani awe amelipa,ikishindikana ntazuia vitu vyake
 
Dah sema wenye nyumba wanakuwaga wababe sana huwa wanaona wameyapatia maisha. Halafu watoto wao wakina kuwa wakubwa wanapitia madhila Yale Yale waliyopitia wapangaji wao. Kama unaweza msamehe tu nyumba hayiami utapata mpangaji mwingine.
mkuu nimemvumilia Sana, hila yote kwa yote inawezekana, maana Bora tu Banda langu hawezi ondokanalo, ikifeli nitamsamehe tu
 
Weka na mlinzi baada ya kumfukuza maana ukinifanyia mimi hivyo nakuja usiku navunja naiba vitu vyote alaf asubuhi naenda kukopa hiyo laki 6 yako nakuletea alaf nakudai vtu vyangu vyenye thaman ya 1.5M+ hapo ndo utauona moto
 
Hiyo ni mahakama gani? mkataba unasemaje?
 
Kosa alilofanya huyo nikufunga nyumba bila yakuwepo huyo mpangaji wake,

Kisheria nadhani wajumbe au mabalozi wanatambulika na mahakama katika suala la Ushaidi,
Kwaiyo boss unashauri njia gani ni nzuri labda
 
Weka na mlinzi baada ya kumfukuza maana ukinifanyia mimi hivyo nakuja usiku navunja naiba vitu vyote alaf asubuhi naenda kukopa hiyo laki 6 yako nakuletea alaf nakudai vtu vyangu vyenye thaman ya 1.5M+ hapo ndo utauona moto
ukija kuvunja unatengeneza kesi ya ujambazi Sasa πŸ˜ŽπŸ˜‚
 
Una mkataba nae wa maandishi? Uliupitisha tra na unalipa Kodi? Kama mna makubaliano ya mdomo Bora uondoe kimyakimya maana anaweza kusema humdai na ukashindwa kuthibitisha.
 
Una mkataba nae wa maandishi? Uliupitisha tra na unalipa Kodi? Kama mna makubaliano ya mdomo Bora uondoe kimyakimya maana anaweza kusema humdai na ukashindwa kuthibitisha.
Yaan mkataba wa nyumba kupangisha upitishe Hadi TRA, nayeye akisema simdai si aonyeshe Ushaidi,

Nna Ushaidi wa kieletronic kuwa namdai na anafahamu
 
Sasa akianza kuhamisha vitu vya thamani mwezi ukifika akuachie masufuria.Hapo ni kumkazia sa hivi haina kusubiri,deni linazidi kuongezeka na uwezo hana.
hapo ndio hofu yangu,mnaandikishiana, usiku anahamisha vitu vya thamani anaacha masufulia tu anahama
 
Ahahah,Kama ni chumba kimoja kinajitegemea unaweza kufanya hivyo πŸ˜‚
 
Nikweli,inabidi niendenae taratibu tu, ngojea nimuandikie NOTICE kwamba Hadi muda fulani awe amelipa,ikishindikana ntazuia vitu vya
Ni naona mpe notisi ya miezi mitatu

Deni mwambie ukiona ni haki yangu utanilipa ila ukiona siyo haki yangu basi kaa nayo .

Ili uweke mpangaji mwingine upate pesa.

Ukiendelea kung'ang'ana naye huyo ndugu unajichelewesha .
 
Kama uwezo hana mzee kua muungwana maisha yanabadilika sana ukute anawaza namna ya kumaliza deni lako ingekua uwezo upoo labda hapo ungewaza ufanye nini
kulipana hivo ni changamoto sana,hapo akimaliza deni ina maana miezi inakimbia pia na miezi inayokuja Mambo yale yale deni lingine linaanza
 
Nenda taratibu. Ni wanadamu wanakwaza.

Mie nina wa kwangu namdai karibia kodi ya miezi 8. Nasikia anajinasibu kwa wenzie anasema
"YAANI NIACHE KUMLIPIA MWANANGU ADA, NIMLIPE HUYO BOYA, FALA KODI YAKE..."

Namvutia pumzi
 
Ni naona mpe notisi ya miezi mitatu

Deni mwambie ukiona ni haki yangu utanilipa ila ukiona siyo haki yangu basi kaa nayo .

Ili uweke mpangaji mwingine upate pesa.

Ukiendelea kung'ang'ana naye huyo ndugu unajichelewesha .
umeongea point mkuu,

Ntalifanyia kazi, Baada ya kuandika notice, Kuna haja yakumpa then nikabakia na copy yake
 
Nenda taratibu. Ni wanadamu wanakwaza.

Mie nina wa kwangu namdai karibia kodi ya miezi 8. Nasikia anajinasibu kwa wenzie anasema
"YAANI NIACHE KUMLIPIA MWANANGU ADA, NIMLIPE HUYO BOYA, FALA KODI YAKE..."

Namvutia pumzi
Dah,aisee mtu Kama huyo inatakiwa kumfanyia tu umafia wa aina tofauti
 
kulipana hivo ni changamoto sana,hapo akimaliza deni ina maana miezi inakimbia pia na miezi inayokuja Mambo yale yale deni lingine linaanza
Na ndio inakoendea Sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…