Akifanya hivyo atakuta chumba kitupu mkuu
Ni heri tu ahame atafute mpangaji mwengine amlipe kodi.
Nakumbuka nishakuwaga na Mpangaji akapata changamoto ya ugonjwa alikonda jamaa hadi kitaa wakawa wananiambia yule mpangaji wako ameungua.
Jamaa alichoka kazi zake zikakwama mke wake akaondoka na vitu Kama vyote akaenda kwao.
Kodi yake ilipoisha akawa hana uwezo wa kulipa, ukapita mwezi wa 1,2,3 ananipiga sound ila nilikuwa na Mimi namuonea huruma flani kodi yake ilikuwa laki 2 kwa mwezi.
Nikaona isiwe tabu nikampeleka kwa Mtendaji wa Mtaa, akaitwa kwa barua tukaenda jamaa akasema hayupo vizuri na pia ni mgonjwa ,kaenda hospital I ugonjwa hauonekani.
Dah unaambiwa alikuwa anatia huruma.
Mtendaji akamwandika notisi ya mwezi ahame na anilipe kodi anazodaiwa au alipe kodi Kama kawaida ya miezi 6.
Mwezi wa notisi ukaisha jamaa hana kitu nikaenda kumripoti kwa Mtendaji ,Mtendaji mwenyewe akawa anamuonea huruma jinsi anavyoumwa yaani we acha .
Dunia Ina majaribu Sana, Mtendaji anamkoromea jamaa anamwambia kesho nakuja na mgambo kukutoa kwenye hiyo nyumba jamaa anabaki analia , anaambiwa haya nenda kesho ujiandae tunakuja kukutoa.
Mtendaji ananiambia nibaki ,Mtendaji ananiambia nimsikilizie jamaa ni mgonjwa akija kumtoa anaweza asieleweke na jamii. Na Mimi nikawa namkubalia tumsikilizie ikawa ndio hivyo had ikafika miezi 4 Mtendaji anasita kumtoa.
Kuna siku na hasira zangu nikapiga zangu konyagi za kutosha nikasema wacha nikamtoe yule Mpangaji Mimi mwenyewe Mtendaji anazingua.
Nikaenda pale kwangu had I anapoishi nasikia ndani jamaa anakohoa kugonga anauliza wewe nani namjibu mwenyewe nyumba ananiambia ingia ndani.
Dah kuingia ndani nikakuta jamaa alikuwa anatapika kishenzi ndani ya ndoo nyumba chafu jamaa anakitanda nagodoro tu nikamwambia we jamaa unataka kufia hapa kwangu nini. Halafu na kodi hulipi unataka kunipa mzigo nini.
Unaambiwa jamaa akawa analia akaniomba nauli aende kijijini kwao.
Nikashikwa na huruma nikampa elfu hamsini nikamwambia na kodi yangu nimekusamehe .
Kweli jamaa kesho yake tu akatoa vitu vyake akataka kuviuza akakosa mteja akasepa akaviacha nje.
Ikabidi niviweke stoo vitu vyake nikapiga rangi nyumba nikapangisha mtu mwingine.
Baada ya Kama mwaka jamaa alikuja kunisalimia Bahati nzuri akanikuta alikuwa amenawiri amepona yupo fresh,
Aliniambia alivyokwenda kijijini kwao ikaonekana alikuwa ametupiwa majini na ndugu yake hivyo wakamfanyia matibabu akapona.
Jamaa alinishukuru Sana akaniambia amekuja kunilipa kodi niliyokuwa na mdai Yaani bila kutegemea nikala laki nane.
jamaa hadI Leo rafiki yangu.
Kwenye haya maisha kuna watu wanapitia mitihani mikubwa Sana si vyema kumcheka,kumdharau au kumnyanyasa mtu ni swala la kumshukuru Mungu kila wakati Kama amekujalia kuepukana na dhiki ,karaha, na magonjwa.