Naomba ushauri: Mpangaji wangu msumbufu kulipa kodi nataka nifungie vitu vyake

Dah sema wenye nyumba wanakuwaga wababe sana huwa wanaona wameyapatia maisha. Halafu watoto wao wakina kuwa wakubwa wanapitia madhila Yale Yale waliyopitia wapangaji wao. Kama unaweza msamehe tu nyumba hayiami utapata mpangaji mwingine.
Sawa kabisa mimi jamaa alishindwa kunilipa shg. 1,500,000/= . akahama na sikumdai mpaka leo. Nyumba ikapata mpangaji mwingine na maisha yanaendelea. Hakuna haja ya kugombana maana akihama nyumba ipo tu.
 
Mwambie ahame kwa nyumba yako, inaonekana huyo mpangaji ameshakua sugu sana hapo mahali, na hawa watu wanajua mahali pa kuchezea akishakuona makubaliano ya Kwenye mkataba

alishayavunja na wewe mwenye nyumba ukaona sawa tu..ndio hapo wanaanza kizungumkuti, anajua kabisa huyu jamaa anaongea hivi lakini hatekelezi anachosisitiza, Mzozo wote ulianzia kwenye mkataba ambao uliingia nae, kwamba kodi inayofuatia ilipwe siku kumi na tano kabla ya muda wake wa kupanga kuisha, yani dhamani ya hiyo huioni tena sababu ya vichaa kama hawo.
Pole mkuu.
 
Nenda taratibu. Ni wanadamu wanakwaza.

Mie nina wa kwangu namdai karibia kodi ya miezi 8. Nasikia anajinasibu kwa wenzie anasema
"YAANI NIACHE KUMLIPIA MWANANGU ADA, NIMLIPE HUYO BOYA, FALA KODI YAKE..."

Namvutia pumzi
Watu wana roho za ajabu mpaka unajiuliza kama mungu yupo mbona anaruhusu roho kama hizo kuwapo.
 

Daah mkuu hayo maeneo uliyotaja yamejaa dhiki, ufukara na umasikini ulioambatana na laana kali sana.
 
Unayomdai msamehe. Achana nayo. Ila tu mwambie ahame mpe hata wiki aondoke
 
Samahani kidogo, ulikua unamdai milioni moja na laki mbili...akalipa laki nne ikabaki laki sita, hizo laki mbili nyingine mlikubaliana vipi?
Hiyo milioni 1.2 umeikuta wapi mkuu?
 
Kuna jamaa mmoja aligonga mpangaji wake, mpangaji akajilenga na kamimba juu. Kutoa mimba hataki, kuhama nyumba hataki na kulipa kodi hataki.
 
Kama uwezo hana mzee kua muungwana maisha yanabadilika sana ukute anawaza namna ya kumaliza deni lako ingekua uwezo upoo labda hapo ungewaza ufanye nini
Hiyo ni biashara kama zingine
 
nimesoma nikacheka kwakuwa kwanza ninakimeo cha kodi cha mwenye nyumba wangu ambaye naenda kumpanga muda si mrefu.
vumilia korona mwisho mwaka huu harafu zitaingia Subaru mambo yatakuwa sawa na hizi tozo ndo kabisa!
 
Hii ndio nzuri
 
Yaan mkataba wa nyumba kupangisha upitishe Hadi TRA, nayeye akisema simdai si aonyeshe Ushaidi,


Nna Ushaidi wa kieletronic kuwa namdai na anafahamu
Hujui kuwa mkataba inabidi uende Tra ulipiwe withholding tax na stamp duty?
 
Leo zamu ya wenye nyumba kunanga wapangaji!
 
Mvumilie tu atakulipa au njoo na trekta vunja mabanda yako atahama kwa urahisi sana. Au kunya mavi weka mlangoni mwake atahama haraka.
 
Huu uchumi wa kati umekuja na changamoto kibao kwa wapangaji hasa ukizingatia uchumi wa tokea jiwe hadi sasa uchumi wa tozo, mwambie kama anataka kuendelea aonyeshe commitment kabla mkataba haujaisha....
 
Hakuna Cha kuachana nae mkazie tu kwa namna yoyote. Ujenzi ata Kama ni banda unapasua vichwa. Makazie kabisaa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…