Naomba ushauri: Mpangaji wangu msumbufu kulipa kodi nataka nifungie vitu vyake

Kama ana lewa au anakaanga maini na firigisi hizo zitakua dharau chujua hatu ila kama ila kama anakula mlo mmoja au miwili kwa siku msamehe
 
Unayomdai msamehe. Achana nayo. Ila tu mwambie ahame mpe hata wiki aondoke
Atataka notisi ya mwezi sijui mitatu, hao jamaa wanakuwaga sugu halafu wazoefu wa dhulma, na sheria wanazijua...jichanganye tu ndio utawajua..
 
Asante kwa ushuhuda huu...
 
Usije ukampangisha mtu asiye na kazi ya kueleweka.
Machinga, mama ntilie na wabangaizaji wote iwe no go zones.
Nilitaka kusahau.
Usije ukampangisha policcm au mmakonde au muha au mpemba.
 
Kama uwezo hana mzee kua muungwana maisha yanabadilika sana ukute anawaza namna ya kumaliza deni lako ingekua uwezo upoo labda hapo ungewaza ufanye nini
Ukute pia alikuwa mpangaji wake kitambo tu nahakuwa anasumbua malipo ya kodi, huwenda ikawa mpangaji wake upepo wa hela ndio umekaa vibaya tu
 
Somo zuri sana
 
Fanya kazi acha kutegemea nyumba ya urithi
 
Nenda kwa mwanasheria amwandikie notisi ya kuondoka kwenye nyumba yàko kwa kigezo labda unataka kufanya ukarabati mkubwa. Nadhani kodi ya mwezi mmoja itabidi umwachie wakati akitafuta nyumba. Ila na mwanasheria naye utampa ada kidogo. Niliwahi saidika kwa namna hiyo
 
Fasiliteta... Mood yako nmeielewa boss, kweli maisha hubadirika sidhan kama huyo mpangaji anafanya ubabe kutolipa kodi pengine tu ni hali ya uchumi haijawa OK Ila hataki tu kuwa wazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…