Pacbig
JF-Expert Member
- Oct 15, 2017
- 1,095
- 2,087
Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu mwaka wa pili nimekuwa mtu mwenye personality inayobadilika sana kwenye maisha yangu.kuna kipindi nilikuwa mtu mchangamfu na muongeaji sana specifically kuanzia primary level mpaka form two ila kuanzia form three mpaka leo nimekuwa na aibu aibu na mpole na ninapenda sana kukaa peke yangu kuliko kuchangamana ila ninajiamini kupita kiasi ikitokea isue serious natakiwa kuifanya na kuikamilisha.
Mwanzoni nilikuwa siipendi hii tabia but kwa sasa nimeikubali na nimeamua kuishi hivyo ikiwezekana maisha yangu yote.Ila kuna tabia ya watu kupenda kunipambanisha(compare) na watu wengine mara we mpole unazidiwa ujanja na fulani vitu ambavyo sina mda navyo kabisa.Watu wengi wanaonipambanisha wanataka nibadilike lakini mimi siwezi kabisa.
Kilichonifanya nije hapa hasahasa kuna girlfriend wangu anachukia pia nilivyo mpole ila ananipenda sana na yeye ni mcharuko balaa nahisi anaweza kuniacha na sipendi hilo litokee .Mbali na hilo hata ndugu sometimes wanaonyesha kutonijali japo hili haliniumizi sana kwa sababu hata wasiponijali mimi naona safi tu.Je nifanyeje sipendi kumpoteza huyu mwanamke na ninapenda kuwa karibu na ndugu zangu lakini napenda sana pia haya maisha ninayoishi.Naomba ushauri?
Mwisho nina swali kwa wanaojua saikolojia ili niongeze uelewa je personality inachangiwa na nini kubadilika?
Karibuni wakuu.