Naomba ushauri na Majibu kuhusu hii personality yangu isiyopendwa na wengi

Pacbig

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2017
Posts
1,095
Reaction score
2,087
Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu mwaka wa pili nimekuwa mtu mwenye personality inayobadilika sana kwenye maisha yangu.kuna kipindi nilikuwa mtu mchangamfu na muongeaji sana specifically kuanzia primary level mpaka form two ila kuanzia form three mpaka leo nimekuwa na aibu aibu na mpole na ninapenda sana kukaa peke yangu kuliko kuchangamana ila ninajiamini kupita kiasi ikitokea isue serious natakiwa kuifanya na kuikamilisha.

Mwanzoni nilikuwa siipendi hii tabia but kwa sasa nimeikubali na nimeamua kuishi hivyo ikiwezekana maisha yangu yote.Ila kuna tabia ya watu kupenda kunipambanisha(compare) na watu wengine mara we mpole unazidiwa ujanja na fulani vitu ambavyo sina mda navyo kabisa.Watu wengi wanaonipambanisha wanataka nibadilike lakini mimi siwezi kabisa.

Kilichonifanya nije hapa hasahasa kuna girlfriend wangu anachukia pia nilivyo mpole ila ananipenda sana na yeye ni mcharuko balaa nahisi anaweza kuniacha na sipendi hilo litokee .Mbali na hilo hata ndugu sometimes wanaonyesha kutonijali japo hili haliniumizi sana kwa sababu hata wasiponijali mimi naona safi tu.Je nifanyeje sipendi kumpoteza huyu mwanamke na ninapenda kuwa karibu na ndugu zangu lakini napenda sana pia haya maisha ninayoishi.Naomba ushauri?

Mwisho nina swali kwa wanaojua saikolojia ili niongeze uelewa je personality inachangiwa na nini kubadilika?

Karibuni wakuu.
 
Hivi punde ntakuja nikuhabarishe kuhusu psychology hlo tatizo lako ni lakipsychology
 
Personality kubadilika inaweza kua triggered na kitu chochote mfano Jefrey Dahmer (serial killer) alikua na personality zaidi ya moja lakini nyingine iliweza kua triggered na kitu kidogo mfano akiona haukubaliani na anachotaka.

Ishu yako sidhani kama ni personality disorder kwakua umesema mwanzo ulikua mchangamfu ila baadaye ukawa mpole, na haujasema kama kuna kitu chochote kilichopelekea huo upole.

Ingawa kuonyesha kutojali ndugu zako wanavyokuwazia siyo dalili nzuri lakini hii ripoti yako inahitaji nyama zaidi ili mwanasaikolojia aweze kuamua kama una multipersonalities.
 
Mkuu mimi sio Psychologist ila katika pitapita zangu nimesomasoma kuhusu psychology.Kwanza nilihisi wewe ni melancolin ambalo ni kundi la watu wapole,wenye akili sana,wanaofanya fikra pevu kabla ya maamuzi,wenye hisia Kali za kimapenzi,aibu etc.lakini nimeshindwa kukuweka hapa kwa sababu unaonekana unajikubali sana ulivyo lakini melancolin huwa hawajikubali na hili linathibitishwa na wewe kutokupenda kusifiwa na kujisikia kawaida ndugu wasipokujali.hivyo nimeshindwa kukudetemine una sifa za makundi zaidi ya moja.

Personality inaweza kubadilika kutokana na circumstances mbalimbali kama environment ,motivation,mental disorders etc.

Ushauri wangu ni bora kuwa muwazi kwa huyo girlfriend wako aielewe na azoee kwamba wewe ndo ulivyo kama kweli anakupenda hawezi kukuacha.Vilevile unaweza kuona ndugu hawakujali kumbe tatizo lipo kwako wanashindwa wafanye njia gani ili wawe karibu na wewe ukiwa mpole si kila mtu anaweza kukuelewa rohoni mwako wengine wanaweza kukuona wewe ni kauzu tu.jitahidi kuwa karibu na nduguzo kwa kushirikiana nao katika mambo mbalimbali wanaweza kukuelewa.

Mwisho kuhusu wanaokupambanisha psychologically sometimes ukiona mtu anapenda kukupambanisha na watu wengine elewa anafeel inferior mbele yako ujue kuna vitu anahisi unamzidi hivyo anafanya hivyo ili kuku distract your mind.hao ni wa kupuuza tu
 
Umesema mwanzoni ukiwa kidato cha tatu na nne u was so charming but now no longer, what I want from u is that; mabadiliko yako sio ya kawaida kabisaa na huenda ni tatizo la kimazingira au familia pia.
 
nimekupata vyema mkuu ila ningependa kujua hasa kwa nini umesema kutokujali ndugu wanavyoniwazia ni tatizo?

Kingine kuhusiana na sababu iliyonifanya nibadilike kiukweli hii hata mimi sijaielewa vizuri kwa sababu nilichange very sudden ila nachokumbuka nilipokuwa form three nilihamishwa nikaenda kusoma shule moja iko mbeya(mbeya day) nikaenda kusoma nilikuwa nakaa kwa brother angu aliyekuwa ameoa na ndugu wengine kama wawili tunaolingana kiumri.nililazimika kuishi maisha flani ya kishua sana ambayo nilikuwa sijayazoea vilevile member wengine wa familia walikuwa kama wananitenga na ninadhani walikuwa wananichukia kwa sababu brother alionyesha kunikubali sana kwa sababu nilikuwa nafanya vizuri darasani kuliko wao hivyo nikawa nakaa peke yangu peke yangu sana.pengine inaweza ikawa sababu japo sina uhakika
 

Ni tatizo kwakua binadamu ni mnyama na kila mnyama anahitaji kua sehemu ambayo ana-belong. Ndiyo maana unakuta kuna waumini hata waambiwe kiongozi wao siyo mkweli wenyewe hawataamini na wataendelea kumfuata.

Unanimaanishia kukosa upendo na ushirikiano kutoka kwa members wengine ndiyo kukapelekea uwe mkimya na mpole?

Kwanini haukuweza kuwa mchangamfu na mcheshi kila ulipokutana na wanafunzi wenzako?

Una hasira na hao members wa familia waliokua wanakutenga? Kama ndiyo, ni kwa kiasi gani? Mfano ukiona nyoka anataka kumgonga utamshtua?

PS. Nimesoma Saikoloji ila sijawahi kwenda field yawezekana kuna clues nazikosa hapa kwenye maelezo yako.
 
Ushauri mzuri kwake
 
Nimekupata vyema sana mkuu shukran sana.
 
Umesema mwanzoni ukiwa kidato cha tatu na nne u was so charming but now no longer, what I want from u is that; mabadiliko yako sio ya kawaida kabisaa na huenda ni tatizo la kimazingira au familia pia.
Ofcourse I used to be charming, kiukweli hata mimi ninakoswaga sababu hasa iliyonifanya nibadilike but kuna point naiwaza sana kuhusu umri je age haiwezi kuchangia mtu kubadilika kweli.kuna matatizo ya kifamilia na kimazingira but ni madogo madogo sana sidhani kama yanaweza kupelekea hilo.
 
Hilo la kukoswa ushirikiano kwa ndugu nahisi limepelekea lakini kuhusu wanafunzi wenzangu labda niweke clear hili mwanzoni nilikuwa nakuwa mkimya sana home shuleni kawaida ila baadae nikaanza kuwa hivyo hadi shule.Sina hasira nao saana hao family member kiasi cha kuwaacha wagongwe na nyoka japo siwezi kusema uongo kiukweli siwakubali kitu kingine kuhusu mimi mtu ukionyesha kunichukia au kutonikubali hata mimi nakuwa sina habari na wewe.
 
Wewe ni MELANCHOLY, aina ya temparament! Google.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…