Naomba ushauri na mawazo kwenye kilimo na ufugaji

Naomba ushauri na mawazo kwenye kilimo na ufugaji

Mheshimiwa nakupongeza kwa kuamua kujichimbia kwenye kilimo wakati ukiendelea kufaidi pensheni yako! Nilivyokuelewa unataka kujiajiri kwenye Kilimo/ufugaji! Naamini mchango wangu wa mawazo kama utakuwa umechelewa kwako utawafaa wanaJF wengine!

Kwa kuwa unajiajiri unapaswa kufanya kibiashara zaidi upate faida zaidi ili kipato kisikatike! Kwanza awali ya yote nakubaliana kuwa hakuna lisilowezekana duniani na tunashauriwa tuepuke kusema kwamba 'jambo hili haliwezekani'! Hata hiyo orodha yako ndefu ya mazao na mifugo inawezekana ni vigumu kuitekeleza! Naomba tu nikushauri yafuatayo ili usije kuingia kwenye mazingira ambayo huwapa kuchanganyikiwa wastaafu wakaishiwa pesa na kuishiwa nguvu mapema sana.

Ndugu yangu orodha yako imenifurahisha imenionyesha kuwa wewe ni mkereketwa hasa wa kilimo na unashauku kubwa ufanye kitu kikubwa. Mimi ninakuunga mkono iwapo dhumuni la uwekezaji wako huo ni kutengeneza kitega uchumi cha utalii (touristic attraction) yaani Agricultural Tourism! Kulinagana na eneo ulilopo kama ni ukanda wa watalii unaweza kuzoa pesa kwani watalii wengi pia hupenda kutazama jinsi gani tunasitawisha mazao na wengine hawajawahi kuyaona! Unaweka uzio kisha unajitangaza watalii wakija wanalipia. Nchi nyingi wanafanya hivyo. Na ndiyo hapo tu ninaafiki wazo la wachangiaji wengine kwamba uongezee na nyuki na samaki!

Pia wazo lako hili ni murua sana iwapo umedhamilia kuanzisha kituo cha mafunzo ya kilimo ambapo utakuwa na mkusanyiko mkubwa wa mazao na mifugo. Hili napo itabidi ujiulize iwapo watanzania wako tayari kulipia mafunzo ya kilimo maana hadi sasa sijaona mfanowe Tanzania!

Lakini tukija kwenye upande wa uwekezaji ili upate faida itakayokufanya uendeshe maisha yako kama zamani ninaingiwa na wasiwasi sana! Kama dhumuni ni kuzalisha kwa ajili ya faida ninawasiwasi sana! Kwa ujumla inategemea na malengo yako na madhumuni yako! Mimi ninajichimbia kwenye eneo moja tu hapa la uzalishaji wenye tija. Orodha uliyokuja nayo hapa ni ndefu sana kwa mtu aliye serious anaetaka kuzalisha kibiashara kwa faida na kipato ili awezekuishi kwa furaha na maendeleo! Haijalishi utastaafu ukiwa na pesa nyingi kiasi gani jua kuwa hiyo pesa utaitandaza kwenye hiyo miradi yote hivyo ufanisi wa mtaji utapungua tofauti na kama ambavyo ingekuwa iwapo ungejimbia mtaji wako kwenye mazao machache na mifugo aina chache tu!

Utaalamu na uzoefu unaonyesha kuwa kadri unavyozidisha mazao tofauti (enterprise) mara nyingi ufanisi katika kila enterprise moja moja hupungua na gharama za uendeshaji huongezeka sana. Kama ukizidisha sana basi inashauriwa usizidi mchanganyiko wa mazao matatu labda na mifugo aina mbili au tatu hivi! Kwa sababu kuzalisha kitu ambacho hujawahi kuzalisha kunahitaji kujifunza mambo mengi sana ambayo huyajui! Unapoingia kwenye uzalishaji inapokuwa ni mara ya kwanza wewe ni kipofu tu, kuna mengi huyajui, sasa utajifunza vitu vingi kiasi hicho kwa wakati mmoja? Halafu bado upate faida? Linapokuja suala la kulima au kufuga watu wa kawaida hudhani ni kutafuta mbegu na kupanda tu, au ni kununua mifugo na kujenga mabanda tu na kuku wa kienyeji wataokota panzi ni hapo utakaposhangaa hata kuku wa kienyeji usipowaendea vizuri huwa wanadunda! Ukishaingia kwenye shughuri yenyewe unakutana na mambo ya kujifunza kwa hasara kubwa! Sasa utapata mafunzo kwa hasara kwenye mazao yote hayo na mifugo yote na ufugaji wa samaki na nyuki ukabaki salama kweli?

Nina mifano mingi nikupe mmoja, rafiki yangu alivutiwa na kilimo cha mihogo baada ya kupiga mahesabu na kuona kinafaida kubwa sana. Akaenda kulima mihogo ikastawi! Mwezi wa Ramadhani ukafika akaenda kuvuna na wanunuzi, mihogo ikatoka mikubwa sana, wafanya biashara wazoefu walipoioa ile aina ya mihogo pale pale wakampa pole! Kila mhogo alioung'oa ulipovunjwa ndani kuna ringi ya nyuzi nyuzi! Yaani ile mbegu aliyotumia ilikuwa haifai eneo lile inatoa nyuzi nyuzi! Walimuelekeza mbegu nzuri kwa eneo lile naye alikiri kuwa alipata shule kwa gharama kubwa! Hali iko hivyo kila tunapoingia zao jipya sasa fikiria una mazao 13 usiyoyajua na mifugo aina 8 usiyokuwa na uzoefu nayo!

Utahitaji umakini sana kujua zao gani linamchango mkubwa na faida kubwa na lipi linanyonya mengine, na mifugo kadharika! Unapokuwa na mazao mengi sana na aina nyingi za mifugo mara nyingi ufanisi unakuwa mdogo sana utajikuta unautaalamu wa kila zao na mfugo kwa juu juu tu! Kuku wa kienyeji pekee yake wanatabia za ajabu ajabu nyingi sana ambazo usipojua kuzidhibiti uzao hauongezeki. Ukijisambaza kwenye miradi mingi (mazao na mifugo) kwa mara moja utaisambaza pesa yako halafu taratibu utaanza kugundua miradi mingine inakusumbua kuiendesha na utaanza kuitelekeza! Kwa ufupi orodha hiyo ni ndefu sana tusitafune maneno haitekelezeki isipokuwa kama ni kwa maonyesho tu ya watalii au kufundishia lakini siyo kwa uzalishaji wenye faida ya kweli!!

Kama ingelikuwa ni kijana anaeingia kwenye shughuri hii angeshariwa aanze kidogo kidogo na kuendelea kujipanua na hatimae angepima iwapo angeendelea kujitanua hadi awe na mchanganyiko mkubwa hivyo! Kwako wewe kama mstaafu jaribu kujipima mwenyewe! Ndiyo maana kwa kuona kwamba unaonekana kupenda mchanganyiko mkubwa wa miradi ukashauriwa ufuge na nyuki na samaki pia! Mheshimiwa ukifanya hivyo utatuachia cha kujifunza duniani kuwa mtaka yote hukosa yote! Tafakari sana!

Samahani sana kwa maelezo marefu saa zingine mimi nami mweeeee!! Heshima kwako Mkubwa Malila nipo kijana wako hapa!!

Kubota nimependa maelezo yako-yana leta sense sana
 
Endelea kutupa taarifa kadiri unavyo piga hatua ndugu. Hakika umechagua fungu jema, Kama mnataka mali mtayapata shambani...
Nami niko njiani, nataka kufanya Kilimo & Ufugaji pia. Kua maskini ukiwa Tanzania ni DHAMBI KUBWA MNO!!
Kweli tupu.
 
Waheshimiwa habarini za kazi!!

Baada ya kutumika serikalini n akwenye mashirika mengine nimeweka mkakati wa kujiajiri ifikapo 2015 na nimedhamiria kujikita katika KILIMO NA UFUGAJI!
KILIMO
Katika kilimo nataka kujishughulisha na mazao yafuatayo
1. Mahindi na Mpunga
2. Mihogo
3. Matunda ( Maembe, Mananasi, Mapapai)
4. Pilipili (Hoho, Pilipili Kali (Pilipili ndefu na pilipili mbuzi)
5. Mboga (Nyanya, Vitunguu, Carrots)
6. Uyoga
UFUGAJI
Katika sualal la ufugaji natarajia kujishughulisha na ufugaji wa:-
1. Ngombe wa Maziwa
2. Mbuzi wa Maziwa (wanaozaa mapacha)
3. Nguruwe
4. Kuku wa kisasa (Nyama na Mayai)
5. Kuku wa Kienyeji
MAANDALIZI

Mpango wangu ni kuanza operations ifikapo January 2015, lakini nimejiwekea malengo ya kuanza maandalizi (mfano kutafuta mshamba, kufanya utafiti, kuandaa zana na maeneo ya kazi, kuimarisha mtaji etc) kuanzia January 2013 hadi Dec 2014.
Kwa sasa nimeanza kukusanya taarifa muhimu na “kujipanga” kwa ajili ya utekelezaji huo. N akwa kuwa nipo katika mchakato huu naomba msaada wa mawazo kwa wakle ambao tayari wapo kwenye shughuli za namna hii (iwe ni taarifa za mahitaji, wapi pa kupata msaada wa kitaalamu, contacts za wahusika au hata kama kuna mtu Mwenye documented project sample ya related project anisaidie ili nianze kujipanga). Najiandaa pia kufanya ziara kati ya March na May 2013 kenye maeneo mbalimbali ambako kunafanyika miradi kama hii (miradi midogo na ya saizi ya kati) ya watu mmoja mmoja au vikundi ilki kujipa elimu kwa vitendo!! Naomba wenye uzoefu wawasisiane name kwa email ya SELUDM2012@gmail.com au wani-PM humu tuweze kujuzana! Watakaotoa maoni kupitia thread hii nao pia nitawashukuru! Ahasanteni

Kuhusu ufugaji soma hapa SEKTA YA MIFUGO TANZANIA
 
Back
Top Bottom