ninakushauri, kwa njia rahisi ambayo mahakama haitakuwa na jinsi ila kufanya ombi lako, utafute wakili wa kujitegemea, aandike barua kuwa anaata kukuwakilisha mahakamani, sasa mawakili wa kujitegemea do not appear in Primary courts, hivyo unataka kuhamisha kesi yako toka primary court ambako mawakili hawafanyi kazi ili iende district ambako mawakili huwa wana appear. kwa njia hii, mambo yataenda haraka, la sivyo ukiwa unachelewa, maamuzi yanaweza kufanywa haraka juu ya kesi yako ili ukandamizwe kama wakistuka kuwa unataka kuhamisha kesi. hii ni njia ya haraka na nyepesi ambayo nimeona watu wanatumia. kuna njia nyingine ambazo siwezi kukuambia kwasababu huwa sio productive sana kwasababu mahakama za mwanzo mara nyingi huwa zinaweza kutumiwa vibaya sana na watu wenye pesa waka delay au kusambaratisha haki ya mtu chapchap hasa pale wanapoona unataka kuwawahi. huwezi amini, kuna baadhi ya mahakama za mwanzo nilishawahi kufanya uchunguzi, hata kesi za jinai za watoto zinafikishwa mahakama za mwanzo bila hata kupitia polisi, na zikifika pale mahakama ya mwanzo, wanaiharakisha mno na kumfunga (uchunguzi ulipofanyika ilionekana kuna wazazi wengine wana ugomvi wa kifamilia, hivyo anabambika kesi halafu anaenda kumhonga hakimu wa mahakama za mwanzo anaendesha kesi haraka kambla hujatulia ameshamfunga mtoto yule au mtu mzima yule)....tulienda polisi, polisi nao wanashangaa kwasababu wamekuwa bypassed. kati ya vitu vinavyotakiwa kufanyiwa restructuring hapa Tanzania ni mahakama za mwanzo. ni kichaka kibaya sana (i am sory to say this).
bofya hapa kujua haki zako
SHERIA KWA KISWAHILI
View attachment 104675
View attachment 104676View attachment 104676