Naomba Ushauri: Nataka kuacha kubeti

ACHA KUBETI..KUBETI SIO KAMALI....BORA UCHEZE KAMALI ILA USIBETI....

Najua huta nielewa ila ukinielewa kidogo inatosha...

Mimi nina elimu kubwa juu ya michezo ya kubahatisha ya mitandao...

Kama unapenda kucheza betting nenda kacheze karata ,au kamali zisizo husisha mashine na hesabu...

Katika mashine na hesabu hauta weza shinda labda dunia iumbwe upya...

Katika kamali za mitaani utashina sababu zinahusisha matukio na si hesabu...
 
Nenda kadiposit wew acha undez
Mpaka Mhindi na Mrusi afirisike kmmke
 
hakuna mtu mdhaifu kama anae shindwa kujidhibiti,..huhitaji muujiza wowote ule ili uache tabia za kipumbavu kama hizo zaidi ya COMMON SENSE tu.....
 
Kama sio kamali ni kitu gani ?
Anae kuchezesha ukishinda anashinda ukishindwa anashinda...Kasome katika kamali za mashine kuna kitu kinaitwa Margin ukijua maana ya margin utaacha kubeti kwa mifumo inayo husisha compyuta....... bora ukacheze karata kitaaa....
 
Amua tu kuacha yani ni uamuzi.
Mimi nilikuwa nabet sana ila niliamua siku moja tu kuwa naacha kubet baada ya kupigwa ela ndefu.
Nina mwaka wa 4 nadhani sijabet tena
 
Anae kuchezesha ukishinda anashinda ukishindwa anashinda...Kasome katika kamali za mashine kuna kitu kinaitwa Margin ukijua maana ya margin utaacha kubeti kwa mifumo inayo husisha compyuta....... bora ukacheze karata kitaaa....
Nadhani ameongelea zaidi kubeti yaani mechi za mpira wa miguu
 

Kwa hiyo mpira ni mashine au hesabu?
 
Kabla ya kufikiria kuacha kubeti nakukumbusha tu leo Barca anacheza na kapewa odds 1.50, Lille kapewa 1.99 na yupo nyumbani, afu Sevilla yeye kapewa odds 1.73 na yeye yupo nyumbani pia. Acha tamaa, weka laki tu
 
Nadhani ameongelea zaidi kubeti yaani mechi za mpira wa miguu
Ngoja nikusaidie....katika kamali za compyuta tukio ambalo linauwezekano mkubwa kutokea linapewa kiasi kidogo cha ushindi na wachezesha kamali...na lile ambalo lina uwezekano mdogo kutokea linapewa kiasi kikubwa...


Wakati katika maisha harisi ya kamali za bila kuhusisha kompyuta mfano za karata...ukiwa mnacheza na binadamu mwenzako...tukio lolote linapewa asilimia 50 ya ushindi...na 50 ya kupoteza

Hiyo ndiyo tofauti.....
 
Hapo nime kupata
 
Kubeti ni dhuruma kama dhuruma nyingine....anayenufaika na mfumo wa kubeti ni mwenye kampuni ya kubeti....Hata hivyo hizi kampuni zimewekwa kukusanya pesa ambazo hazina kazi au matumizi...

Kwahiyo kama unaenda kubeti tafsiri ya kiuchumi hiyo pesa yako haina matumizi ni hela inayo zagaaa...Sawa tu na mtu anaye kwenda kunywa pombe kupata stimu....

Ndo maana unashauliwa kubeti pesa isiyo kuwa na matumizi...

Na wanakwambia kubeti sio kazi....au ajira...

Maana yake betting ni mchezo wa kujifurahisha....

Saa kama wewe unaufanya kubeti ni ajira basi kitakacho kukuta ni msongo wa mawazo,kufirisika...N.k

Watu wanafanya betting kama kujifurahisha...wanatumia hela ambazo hawana kazi nazo...

Kama wewe hela yako inakazi...USIJARIBU....
 
Vipi na sisi tunao nunua utelezi, hela yetu haina kazi pia ?
 
Acha utani wewe.
Kubeti ndio mradi pekee unaohitaji mtaji mdogo Sana. Isitoshe, unajua mikionea ndani ya dakika chache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…