Wateja wapo au ukishaagiza ndio utajua mbele kwa mbeleWakuu kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Nina ndugu yangu anafanya biashara flani kutoka SAUZI sasa nataka kumuomba nimpe mtaji wa kuanzia 1M ili nimuagize TV na Redio kwa ajili ya biashara. Je SAUZI ni sehemu sahihi kwa biashara hiyo?
Kama kuna anayefanya anaweza kunipa dondoo za bei n.k pia kama kuna biashara nyingine halali naweza kufanya inayoweza kunipa faida nzuri?
Mkuu Mo na Wachina wamevuruga biashara ya electronics hasa TVs.Nikiagiza wateja watapatikana tu.
Ni kweli kaka najua,pia zinatofautiana bei kulingana na ukubwa.Pia hakuna biashara ya peke yako.Ni kukomaa tu.Mkuu Mo na Wachina wamevuruga biashara ya electronics hasa TVs.
SingSung wana mpaka flat TVs ambazo unachomeka tu flash la movie tena kwa laki 2 tu.
So unapaswa kujua kwanza uwezo wa kununua wa wateja ndani ya soko lako.