Naomba Ushauri, nataka kuuza kila nilchonacho ili nifungue biashara

Naomba Ushauri, nataka kuuza kila nilchonacho ili nifungue biashara

Michael Ngusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2014
Posts
1,637
Reaction score
463
Habari zenu!

Jamani mimi nina business idea, ambayo tayari nina kila kitu upande wa paperworks na marketing strategies, kwa maana kwamba nina uhakika kampuni itasimama. Shida ni kwamba sina mtaji, hivyo nikafikiria nimrudishe home kwanza mke wangu ambaye pia ni mjamzito, akajifungulie huko na kusubiri mambo yangu yakae sawa,. Plan yangu ni kuuza kila kitu cha ndani kwangu halafu nihamie tu kwenye single room bei chee, kisha niache na kazi ili nichukue mafao yangu baada ya miezi 3, nikijumlisha hizo pesa inatosha kununulia vifaa vya kazi na kurent ofisi mjini, mnanishaurije? niko Arusha.
 
Uwe makini mkuu coz umeanza kwa kutundika ndaluga za utumwa(ajira) usije ukaishia na kujitundika mwenyewe kwenye kitanzi! Otherwise Heko mkuu, usirudi nyuma.
 
Hilo wazo sio njia mbadala,maana usije kuuza hadi mke.

Kwanza ungeeleza vitu vya ndani thamani yake ni kiasi gani?na je hayo mfao ni kiasi gani.
Maana wenzio kwenye mafai wanamiaka hawajayapata,utakuja kuacha kazi na mafao kuyapata ukajuta kwanini umeacha.

Na Je ni biashara ipi unataka kuanzisha.
 
taratibu ni kipindi critical mtoto mdogo afu unaacha kazi bora uwe nao kuwa kwa watu sijui ukweni bajeti inaongezeka na saving huwezi. Kwanini usijinyime mshahara ukaanza kidogo kidogo utapanda taratibu. Btw ukiumwa huitaji msaidizi hadi mwenza unamrudisha shamba??? Joking wish you all the best.
 
Kuna mtu namjua huu mwaka wa 3 anafatilia mafao.Wewe una uhakika wa kupata fasta.
 
pamoja na kuwa biashara lazima uwe risk taker lakin wewe ni mcheza kamali.Usipoangalia unaweza ukachanganyikiwa.

Usiache kazi pia usiuze vitu na usimrudishe mke.Endelea kuzichanga kwanza maana nilichokuona ujajiandaa bado unataka kukurupuka.
 
Habari zenu!

Jamani mimi nina business idea, ambayo tayari nina kila kitu upande wa paperworks na marketing strategies, kwa maana kwamba nina uhakika kampuni itasimama. Shida ni kwamba sina mtaji, hivyo nikafikiria nimrudishe home kwanza mke wangu ambaye pia ni mjamzito, akajifungulie huko na kusubiri mambo yangu yakae sawa,. Plan yangu ni kuuza kila kitu cha ndani kwangu halafu nihamie tu kwenye single room bei chee, kisha niache na kazi ili nichukue mafao yangu baada ya miezi 3, nikijumlisha hizo pesa inatosha kununulia vifaa vya kazi na kurent ofisi mjini, mnanishaurije? niko Arusha.

Unafanya kazi gani?

Kama kazi ya uhakika kwanini usikope mtaji bank uanzishe biashara?

huo mchezo unaotaka kuucheza utakugharimu....
 
pamoja na kuwa biashara lazima uwe risk taker lakin wewe ni mcheza kamali.Usipoangalia unaweza ukachanganyikiwa.

Usiache kazi pia usiuze vitu na usimrudishe mke.Endelea kuzichanga kwanza maana nilichokuona ujajiandaa bado unataka kukurupuka.

Mkuu unampango Wa kwenda Thailand lini?
 
Tumia mshahara wako kukopa benki mkuu angalia business haiko straight
 
Mkuu wazo lako ni zuri sana, moja wapo ya vitu vya kutolea maamuzi magum ni kama hivi, ila nafikiri je umefanya utafiti wa kutosha katika biashara hizo? umeangalia biashara unayotaka kufanya itagharimu mtaji kiasi gani? uko benk una kiasi gani? kumbuka biashara wakati mwingine haiitataji mtaji mkubwa. unaweza kuacha kazi, ukatumia hela ndogo uliyo nayo na hata vitu vya ndani usiuze vyote, unaweza kuuza kidogo uka anza biashara uku ukiwa na mtazamo chanya.

suala la kuacha kazi ni kweli linaletega mawazo sana. hata mimi nilipata shida sana kuacha kazi, kipindi hicho ndipo utasikia watu wanakubeza n.k, pia fuatilia kuona kama kuna uwezekano wa kupata mafao yako mapema kabla ya kuacha kazi. mfano kama mafao ya NSSF wakati mwingine hayachelewi. jiridhishe kwanza kabla ya kuacha kazi. ila kumbuka wazo lako linaitaji maamuzi magumu ambayo ukisha yafanya utakalo kutana nalo liwe zuri au baya ulipokee. usije ikatokea hata siku moja ukayajutia maamuzi yako. nikiwa nimetulia vizuri nitakupa ushauri zaidi muda huu siko sehem nzuri. Mungu akusaidie.
 
ukitaka mawazo mazuri nenda sacos yeyote iliyo karibu ukae na waliofilisika na wakupe sababu,kisha ukae na walio win wakupe sababu hapi utaamua ushike lipi
 
Paper work is far from realistic, kuna Gharama za ziada huwa zinajitokeza wakati wa implementation mkuu ambazo unakuwa hukuziweka kwenye paper yako

Usiwe na pupa mkuu,mambo mazuri hayataki haraka,as long as una dhamira ya dhati mimi nadhani jichange taratibu au kama kuna uwezekano wa kuanza hiyo biashara kwa mtaji mdogo na kuisimamia kwa karibu huku Ukiwa na ajira then fanya hivyo
 
Fuata moyo/akili yako inavyokutuma mafanikio yanahitaji maamuzi magumu
na kutake risk. Mke usimrudishe nyumbani mueleze unavyotaka kufanya naye akubaliane, muishi chumba kimoja mkiwa pamoja.
 
Back
Top Bottom