Southern Highland
JF-Expert Member
- Mar 22, 2017
- 14,938
- 25,405
asante sana kaka ni kweli hii itasaidia sana maana itawaunganisha wakulima na wafanyabiashara walioko sehemu mbalimbali ya nchiMkuu inaweza kuwa msaada sana. Nina mpango wa kuingia shamba muda si mrefu lakini nimekua nikijiuliza sana suala la kupata masoko ya uhakika pale mazao yangu yatakapokua tayari. Unadhani kama mfumo wa online market utakuwepo si itakua rahisi sana.
Cha msingi publicize ufahamike kwa wote wakulima na wanunuzi. Itakua rahisi mengine utakua unaongezea mbele kwa mbele huko.
Ofcoz hiyo ni changamoto, labda maoni ya wadau pia tuyasikilize, au ww pia unamaoni gan mkuuNi wazo zuri sana. Ila nikupe changamoto kidogo kama itakuwa na msaada utaifanyia kazi. Utawezaje kuthibitisha uaminifu na usahihi wa taarifa zinazo wekwa kwenye site yako. Kwa mfano mtu aseme yeye ana uza mazao mfano Mahindi na kumbe ni tapeli. Na Mimi kama mteja ambaye nimepata mawasiliano ya huyo Jamaa kutoka kwenye blog yako nikatumia halaf ikatokea amenitapeli. Kwa ishu kama hiyo umejipangaje?
Kwa mtazamo wangu japo sijajua kama kuna vyama vya wakulima auu wafugaji ambavyo vipo active(yaani kiwe na ofisi, uongozi, na wanachama wake wanajulikana kwa kuanzia majina, wanapo ishi pamoja na aina ya mazao wanayo lima au mifugo wanayo fuga) halafu wewe ukawa una chukua taarifa kutoka kwenye uongozi na ikiwezekana kuingia nao mikataba yenye vifungu kama ikitokea mtu wao amefanya utapeli basi kikundi kitashitakiwa. Nadhani inaweza saidia. Japo hapo changamoto inayo kuja hapo ni uwepo wa hivyo vikundi na kuna gharama KUBWA itakutoka mwanzoni ili kukamilisha hilo. Ila kwa ajili ya kulinda brand ambayo itakuwa ni changa kwa wakati huo kama utapata uwezo nadhani itasaidia. Ngoja tusikie na wadau wengine watashaur vipi.Ofcoz hiyo ni changamoto, labda maoni ya wadau pia tuyasikilize, au ww pia unamaoni gan mkuu
Umeongea point kubwa sana brooWatz tulishakaririshwa kwamba wakulima, wavuvi na wafugaji ni maskini na wasiosoma hivyo daraja lao haliwaruhusu kujua mambo haya ya mtandao. Kila kitu ni kujifunza hata sisi tumejifunza kimtindo hatukuzaliwa wala hatujasomea namna ya kutumia mtandao!(LIFE LONG LEARNING) Halafu katika nchi hii na hata nyingine za afrika watu kama wavuvi, wakulima, na wafugaji ndio walitakiwa kuw ana hela kuliko hata sisi tunaoshinda kwenye viofisi na tai ndefu utadhani tumevaa chatu shingoni. Kwa mvuvi au mkulima au mfugaji serious kupata milioni kadhaa kwa mwezi au baada ya miezi miwili, mitatu ni jambo la kawaida ila mazingira ya masoko bado ni changamoto! Na pengine ndio maana mwenzetu ameona hiyo changamoto na anataka kuigeuza kuwa fursa kw akuitatua!
Ni ambazo kwa kias flan zinaendana lakin kwa stytem itakua tofaut na hiyo ya NINAYO.COM, itakua tofaut nimeingia hapo nimeangalia nmeona itakua tofaut na system yangHivi kumbe message yangu haikufika, niliuliza idea yako ina tofauti gani na NINAYO? [www.ninayo.com]
Wazo zuri sana !!! Changamoto utakayokutana nayo ni kwamba wakulima walio wengi hawajaelewa matumizi ya Internet !!! Lakini waweza kuanza taratibu na wazo lako likafanikiwa !!!
Wazo lako ni zuri, lakini usipuuze tahadhari iliyopewa na hawa wadau. Ni kweli kuwa tecno inatumika mpaka vijijini lakini watu wengi wanatumia hizi smart phones kwa ajili ya kuchat na kujipigia picha tu,(whatsapp na facebook). Hawana habari na mambo mengine.Wakulima wangapi wanatumia mitandao? Au umelenga wakulima wa dar wenye mashamba yao huko kibiti, ruvu,vikindu etc
Naomba namba ako niitunze mkuuwazo zuriiii, mm n mkulima nakuahid kukuunganisha na wakulima wote wa kata yangu!! Tunalima sana mpunga na kitunguu
Ni pmNaomba namba ako niitunze mkuu
Ofcoz Chamsingi ni kuanzisha kampen za kuwaweka sawa na wauelewe huu mfumoWazo lako ni zuri, lakini usipuuze tahadhari iliyopewa na hawa wadau. Ni kweli kuwa tecno inatumika mpaka vijijini lakini watu wengi wanatumia hizi smart phones kwa ajili ya kuchat na kujipigia picha tu,(whatsapp na facebook). Hawana habari na mambo mengine.
Hivyo nakushauri kuwa pamoja na kuanzisha hiyo blog yako hakikisha unatoa elimu kwa hao wakulima na wafugaji ambao watakuwa wateja wako.
Asante sana mkuu tupo pamoja mda sio mrefu ntaweka link hum nikikamilisha kila kituIdea ni nzuri mkuu.
Changamoto zipo katika kila project so usiziogope.Anza kupiga kazi mkuu.
Nitafurahi ukituwekea link hapa, tutakua mabalozi wako.
Sawa nakuchekNi pm
sawa mkuuUme iyona fursa ichangamkie fasta mzee