Naomba ushauri: Natamani kuanzisha bishara ya jumla

Naomba ushauri: Natamani kuanzisha bishara ya jumla

TAJIRI MSOMI

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Posts
496
Reaction score
515
HABARI WANA JAMVI

Nahitaji Ushauri, natamani nianzishe biashara ya Jumla kuuza kitu cha aina moja,mbili au tatu tu,sasa ninajaribu kuangalia kati ya Cement, Mafuta ya kupikia au Sukari; etc; Sehem ya biashara ni DSM, nina godown na Frame tayari, ni sehemu ambayo haina watu wengi but ni jirani na maduka mengine ya rejareja kama vile maduka ya vitu vya vyumbani, hardware na vifaa vya umeme.

USHAURI UNAOTAKIWA
1. Bidhaa gani kazi ya Hizo Tatu niendenazo, na au nyingine kama ipo itaje.....unaponichagulia bidhaa plesea sema sababu kwanini
2. Taja bulk seller or sehem ambapo nitaweza kuimport bidhaa hiyo (If possible na bulk prices zake)
3. Nishauri kuhusu license zinazohitajika na wapi nitapata kwa bidhaa unionichagulia
4. Mbinu ya kuifanya hio biashara iweze kufanikiwa
5. Nitaajiri kijana/vijana kuuza, hivyo naamini bidhaa moja kwangu itakuwa rahisi, kwa schedule yangu naweza kwenga dukani kila siku angalau kwa masaa mawili
6. Ushauri mwingine wowote unaoweza unaoweza kunisaidi kwa biashara hii.

N.B. Mtaji wangu ni kati ya 40m-50m, godown na frame ni langu (Hakuna kodi); please tushauriane hapahapa na sio PM

Nashukuru sana Wanabodi kwa Ushauri Wenu
 
Nikikushauri bila kuona mazingira nitakosea sana,ila kwakuwa nina uzoefu wa kutosha na maduka ya vyakula rejareja, maduka ya mangi haya, ukweli ni kwamba hatuwezi kuchukua bidhaa sehemu yenye kitu kimoja au viwili tunahitaji kupata vitu vingi vinavyohitajika dukani sehemu moja ili kuunganisha usafiri na kutopata usumbufu.

Hivyo mafuta ya kula, no, sabuni, no na bidhaa zote za rejareja sukari hapana, labda uuze mchele jumla, chaguo lingine cement japo sijui mazingira uliyopo.
 
Kwenye bidhaa kama sukari , mafuta ya kula vinabadilika bei haraka sana kwa mzigo wa 50M usishangae anguko la bei likakata hata 5M japo kuna wakati pia yanapanda ukiwa na stock kubwa unapiga pesa , ila havitabiriki vinabadilika sana sana sio sawa na cement
 
Mazingira niliyopo yanakubali kila kitu kuuza, but nahitaji kuspecialize kwenye kitu kimoja -vitatu tu, ili kuwa masta mzuri kwa biashara, natamani kwenye eneo langu mtu akihitaji kitu hicho atazame/afikirie Godown kwangu
 
Asante sana mkuu
 
Kwakua umesema kuna ruhusa ya kutaja bidhaa nyingine mimi nasema fungua depot ya maji (maji yawe haya ya Afya, Hill, Uhai na siyo brand kubwa) na hizi spirit za bei chee double kick na wenzake.

Sijui utahitaji mtaji kiasi gani au leseni zinazotakiwa ila najua hizi bidhaa zina faida sana kutokana na recent nimefanya kazi ya route sales na kampuni fulani ya vinywaji na nimeona hii biashara siyo mbaya.
 
Asante sana Mkuu, kwa input
 
Jamani mbona mmeukimbia uzi wa mtu wa maana sana? Ila utakuta tumejazana kwenye nyuzi za kunyanduana tu. Watanzania tusaidiane vitu vya maana kwanza ndugu zangu
 
Nimekua katika biashara ya mafuta. Biashara ya mafuta ni nzuri ila sasa hivi imekosa mzunguko ikichangiwa na kupanda vitu bei. Biashara ya mafuta kikawaida kila dumu la litre 20 faida haizidi 5k kama upatikanaji wa mafuta huko sahihi sokoni.

Ili mafuta yakupe wafaida unatakiwa ununue inbulk ambapo changamoto ndio inaanza hapo.

Ntakupa mfano umeenda kununua pale korie, wale bila kununua gari ya ndoo 800 hawatoi semi yao kukuletea. Nafikiri ukiitaji pungufu ya hapo itabidi ununue kwa msambazaji wakuu.

Kipindi tunafanya biashara hii tulikua tunaweza kununua dumu la lita 20 hadi 25k miaka iyo kumaanisha kwa mtaji wa million 40 ulikua unauwezo wa kununua dumu 1600. Mfano pia mwaka jana dumu lilikua linauza 70- 80 na kitu kwa mtaji wa million 40 unapata mafuta 500 na kitu. Sasa mafuta yanasomeka 100plus kwa mtaji wa million 40 unapata ndoo 400.

Ni biashara ambayo kila msimu wa mafuta unapoanza mafuta yanapanda bei hii inapelekea mtaji kukua kwa ukwasi faida italiwa na mtaji. Ili ufanye kwa nguvu na raha inakuitaji mtaji mkubwa walau million 100 Kuuza jumla

Kila bei inapopanda inapunguza purchasing power kwa wateja wako. Mfano alikua anatumia million kununua ndoo 10 akikuta zimepanda atatumia million kununua ndoo 8

Bulk sellers wapo kuna kiwanda cha korie pale vingunguti, kuna supplies tu wakubwa hasa wahindi.

Leseni ni kawaida kwa mafuta utaitaji leseni halamshauri, TIN, VAT registration maana mafuta yanamauzo makubwa, Fire watapiga kusumbua, na watu wa chakula na dawa.

Biashara ya kuoanisha na mafuta ni chumvi na sukari.

Faida ipo ndio maana watu wanaendelea kufanya.

Ata sijui naandika nini ila naandika mengi mengi. Utauliza vingine kwa msaada zaidi
 
Mazingira niliyopo yanakubali kila kitu kuuza, but nahitaji kuspecialize kwenye kitu kimoja -vitatu tu, ili kuwa masta mzuri kwa biashara, natamani kwenye eneo langu mtu akihitaji kitu hicho atazame/afikirie Godown kwangu
Good idea kuuza bidhaa moja au tatu ni wazo zuri kwasababu utakua master katika ilo eneo utatengeneza jina
 
SME nikampuni ya uhakika kutoka Marekani inayolipa kwa masaa, kwa siku, kwa wiki, kwa mwezi, miezi hadi mwakaa

Naweza kujiungaje??

Jisajili kwa line yako kisha downlod App ya kampuni utakutana na offa yako ya Tsh 10,000/= iwekeze ukitaka uanze kuvuna faida 🤑🤑

Malipo hufanyikaje??

Malipo yote hufanyika Kwa njia mbili kama ifuatavyo👇

M PESA na mfumo wa USDT Kwa wale wenye Wallet

Vifurushi vyake vikoje??

Baadhi ya vifurushi vyake ni hivii hapa 👇

Ukiweka Tshs 30,000/= utapokea sh. 1440 kila siku kwa siku 7 kwa muda wa wiki 5

Ukiweka Tshs 80,000/= utapokea she 4320/= kila siku kwa mda wa siku 15 kwa muda wa wiki 10

Ukiweka Tshs 200,000/= unapokea shs 12,000/= kila sikuu kwa siku 30 kwa miezi mitano

Ukiweka Tshs 500,000/= Utapokea shs 34,000/= kila sikuu kwasiku 60 kwa miezi 10

Utawekeza tena na tenaa

Withdrawal

Kiwango cha chini cha utoaji ni Tsh 5000/= kwa njia ya m-pesa au USDT

withdrawal fee ni 15%

Jisajiri link

Ingia kwa group 👇
 
Mimi naona ungeuza bidhaa za majumbani mchanganyiko usibase kwenye biadhaa moja tu.
Mfano sukari,mafuta,sabuni,dawa za mswaki,majani ya chai,juice,ngano,mchele n.k.
Halafu unakuwa unawauzia jumla na mtu akitaka rejareja pia unamuuzia nadhani itakupatia wateja sana mfano sukari wewe hutopima robo wala nusu unaanzia kg 1.
Hapo utapata wateja wa jumla na rejareja pia.
Kuhusu wapi pa kupatia bidhaa wajuzi watakujuza.Sio mwenyejinwa huko hivo sijui.
Pia huwa naona kama unachukua mzigo mkubwa Kuna makampuni yanakuletea mpaka dukani mfano dawa za mswaki na bidhaa nyingine.
Hapa sasa kama sehemu fremu ilipo maduka ya rejareja yapo mbali kidogo au sehemu ambayo kuna mzunguko wa watu wengi pia mfanyabiashara wa rejareja anaweza kununua bidhaa kwa urahisi bila usumbufu wa kuzifuata mjini hasa kama mzigo anaoutaka ni mdogo tuseme ameishiwa mfano sabuni ya unga ambayo inauzwa 15000 kuzifuata mjini ni mbali plus gharama ya usafiri hivo itampasa kuichukulia kwako ambapo unaweza kumuuzia 15500 au 1600.
Nadhani pia leseni yake unalipia kama unavyolipa duka la rejareja.Namaanisha gharama zinafanana.Kama nakosea wajuvi watanirekebisha.
Kuhusu TRA sijui.
Kila la kheri ndugu.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
SME nikampuni ya uhakika kutoka Marekani inayolipa kwa masaa, kwa siku, kwa wiki, kwa mwezi, miezi hadi mwakaa

Naweza kujiungaje
??

Jisajili kwa line yako kisha downlod App ya kampuni utakutana na offa yako ya Tsh 10,000/= iwekeze ukitaka uanze kuvuna faida 🤑🤑

Malipo hufanyikaje??

Malipo yote hufanyika Kwa njia mbili kama ifuatavyo👇

M PESA na mfumo wa USDT Kwa wale wenye Wallet

Vifurushi vyake vikoje
??

Baadhi ya vifurushi vyake ni hivii hapa 👇

Ukiweka Tshs 30,000/= utapokea sh. 1440 kila siku kwa siku 7 kwa muda wa wiki 5

Ukiweka Tshs 80,000/= utapokea she 4320/= kila siku kwa mda wa siku 15 kwa muda wa wiki 10

Ukiweka Tshs 200,000/= unapokea shs 12,000/= kila sikuu kwa siku 30 kwa miezi mitano

Ukiweka Tshs 500,000/= Utapokea shs 34,000/= kila sikuu kwasiku 60 kwa miezi 10

Utawekeza tena na tenaa

Withdrawal

Kiwango cha chini cha utoaji ni Tsh 5000/= kwa njia ya m-pesa au USDT

withdrawal fee ni 15%

Jisajiri link

Ingia kwa group 👇
Tuwasiliane
 
Back
Top Bottom