Mimi naona ungeuza bidhaa za majumbani mchanganyiko usibase kwenye biadhaa moja tu.
Mfano sukari,mafuta,sabuni,dawa za mswaki,majani ya chai,juice,ngano,mchele n.k.
Halafu unakuwa unawauzia jumla na mtu akitaka rejareja pia unamuuzia nadhani itakupatia wateja sana mfano sukari wewe hutopima robo wala nusu unaanzia kg 1.
Hapo utapata wateja wa jumla na rejareja pia.
Kuhusu wapi pa kupatia bidhaa wajuzi watakujuza.Sio mwenyejinwa huko hivo sijui.
Pia huwa naona kama unachukua mzigo mkubwa Kuna makampuni yanakuletea mpaka dukani mfano dawa za mswaki na bidhaa nyingine.
Hapa sasa kama sehemu fremu ilipo maduka ya rejareja yapo mbali kidogo au sehemu ambayo kuna mzunguko wa watu wengi pia mfanyabiashara wa rejareja anaweza kununua bidhaa kwa urahisi bila usumbufu wa kuzifuata mjini hasa kama mzigo anaoutaka ni mdogo tuseme ameishiwa mfano sabuni ya unga ambayo inauzwa 15000 kuzifuata mjini ni mbali plus gharama ya usafiri hivo itampasa kuichukulia kwako ambapo unaweza kumuuzia 15500 au 1600.
Nadhani pia leseni yake unalipia kama unavyolipa duka la rejareja.Namaanisha gharama zinafanana.Kama nakosea wajuvi watanirekebisha.
Kuhusu TRA sijui.
Kila la kheri ndugu.
Sent from my Infinix X657B using
JamiiForums mobile app