Naomba ushauri, nimeamua kufanya kilimo kama ajira

wcyra

Member
Joined
Nov 25, 2014
Posts
8
Reaction score
11
Natumaini wote mu wazima wa afya

Mimi ni kijana umri miaka 27. Nilijipa muda wa miezi mitatu niamuae nijiajiri mwenyewe lakini sikujua wapi ingawa nilikuwa na mawazo ya biashara kadhaa.

Mengi yalihitaji mitaji mikubwa na uwezo wangu ulikuwa ni laki tano maximum lakini nilijiwekea tarehe moja ya mwaka huu 2020 saa sita nifanye maamuzi.

Baada ya kuangalia na kuzunguka mjini Iringa na sehemu nyingine nimeona nianze kilimo kama ajira ya kudumu. Kwa miaka mitano ya kwanza nategemea kufikisha hadi heka 20 za mazao tofauti tofauti ya biashara na chakula.

Mwaka huu mwezi wa pili nataraji nitaanza na heka moja ya maharage kwa gharama ya laki nne mpaka kuvuna huo mwezi wa 5. Hiyo ni gharama na ya kukodia shamba.

Pia mwezi wa tano nina plan ya kutafuta eneo la kukodi maeneo ya Kalenga(Iringa) huko nimeambiwa kuna scheme za umwagiliaji. Nako nitaanza na heka moja ya mazao kati ya haya (mahindi ya kuchoma au maharage(njano) au kitunguu maji au nyanya).

Lengo ni kuzalisha kipindi chote cha mwaka.

Nimewaka mada hii kwa lengo la kuomba ushauri kwa wazoefu wa kilimo pia kwa watu wengine kuhusu hili na uzoefu wao katika kilimo pia kwa aliye na uzoefu ya maeno ya Iringa, ni wapi naweza pata eneo la kukodi kwa kipindi hiki na sehemu nzuri kwa kilimo cha maharage?

Lengo kuu ni kuanzisha kampuni itakayo jihusisha na masuala ya kilimo baada ya miaka mitano pia kupata mtaji wa kuanza kufanya biashara nyingine hapo baadaye.

Naombeni ushauri na nasaha zenu wazoefu na kilimo pia watu wengine.
 
Nakusalimu ndugu yangu,
Hongera kwa wazo lako zuri,
Ushauri wangu kwako
Huo mtaji wako ndio mzizi wa utajiri wako weka hilo kwenye akili.yako na endapo utaupoteza kwa uzembe wa kujua au kutokujua lazima itakugharimu na kukkukatisha tamaa ya kusonga mbele

Fanya uchunguzi wa kutosha
Kuhusu zao unalolipendelea fanya field nenda mashambani mwa watu wanaolilima ili uone wao hufanyaje na utapa uzoefu
Weka suti na moka pemben vaa but ingia shambani

Baadae nenda tafuta shamba na ufanye kilimo cha uhakika siyo cha kubahatisha! wcyra,
 
Hongera sana mkuu kwa kuthubutu [emoji123][emoji106]
Kuhusu kilimo cha mahalage kwa mwezi wa pili naona utakuwa sawa maana mahalage ayaitaji joto la chini kwaiyo unaweza kupata mavuno mengi ata ivyo utakuwa na miezi miwili na nusu iv ya mvua Yan 2-4½ itakuwa kitu kizuli sana maana kipindi mahalage yanotoa mauwa inabid mvua isiwepo ili kiluhusu uchavushaji, Kama ukizingatia vizuli kanuni za kilomo yan uwekaji wa mbolea na kupalilia unaweza vuna mazao mengi... Lkn pia sijua Kama utauza kwa plastic au kilo au utatumia madalali



Kwenye upande wa mahindi kwa sababu n ya kuchoma huwa yana chukua miezi 4-5 iv itategemeana na aina ya mbegu yako, tufanye takwimu kidogo
Arce moja ni sawa 70m × 70m =4900m²
Mstali adi mstali 75cm
Mche adi mche 25cm
Jumla ya mimea 26133
Tufanye Kama mimea 133 imekufa kutokana na athali za mazingila kwaiyo itabaki mimea 26000
Kuhusu soko sijajua Kama utauza wakati ipo shamaban maana utamuuzia dalali tufanye takwimu kidogo
Muhindi moja 100 Tsh
Jumla ya mahindi 26000
Mkusanyo wa pesa 2,600,000

Kama utamuuzi mchoma mahindi moja kwa moja tufanye ( yani inabid uvune alafu utafute kituo cha kuhuzia yan ww ndo unakuwa Kama muuzaji mkuu)
Muhindi mmoja 150 Tsh
Jumla ya mahindi 26000
Muhindi mmoja 150
Mkusanyo ya pesa 3,900,000 Tsh



Lkn kama tatafuta sehemu ya kuuzia Yan utauza moja kwa moja kwa mchoma mahindi itakuwa ni vizuli maana yale majan ya nayo funika muhindi uwa yana punguzwa ili kulahisisha usafilishaji kwaiyo unaweza kuyakusanya na kuyauza kwa wafungaji wa Ng'ombe na Mbuzi ivyo basi ukapata faida zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mahindi yapi hayo yanayochukua 4-5 mths mkuu? Ni kilimo biasharbiashara au just kilimo tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…