Natumaini wote mu wazima wa afya
Mimi ni kijana umri miaka 27. Nilijipa muda wa miezi mitatu niamuae nijiajiri mwenyewe lakini sikujua wapi ingawa nilikuwa na mawazo ya biashara kadhaa.
Mengi yalihitaji mitaji mikubwa na uwezo wangu ulikuwa ni laki tano maximum lakini nilijiwekea tarehe moja ya mwaka huu 2020 saa sita nifanye maamuzi.
Baada ya kuangalia na kuzunguka mjini Iringa na sehemu nyingine nimeona nianze kilimo kama ajira ya kudumu. Kwa miaka mitano ya kwanza nategemea kufikisha hadi heka 20 za mazao tofauti tofauti ya biashara na chakula.
Mwaka huu mwezi wa pili nataraji nitaanza na heka moja ya maharage kwa gharama ya laki nne mpaka kuvuna huo mwezi wa 5. Hiyo ni gharama na ya kukodia shamba.
Pia mwezi wa tano nina plan ya kutafuta eneo la kukodi maeneo ya Kalenga(Iringa) huko nimeambiwa kuna scheme za umwagiliaji. Nako nitaanza na heka moja ya mazao kati ya haya (mahindi ya kuchoma au maharage(njano) au kitunguu maji au nyanya).
Lengo ni kuzalisha kipindi chote cha mwaka.
Nimewaka mada hii kwa lengo la kuomba ushauri kwa wazoefu wa kilimo pia kwa watu wengine kuhusu hili na uzoefu wao katika kilimo pia kwa aliye na uzoefu ya maeno ya Iringa, ni wapi naweza pata eneo la kukodi kwa kipindi hiki na sehemu nzuri kwa kilimo cha maharage?
Lengo kuu ni kuanzisha kampuni itakayo jihusisha na masuala ya kilimo baada ya miaka mitano pia kupata mtaji wa kuanza kufanya biashara nyingine hapo baadaye.
Naombeni ushauri na nasaha zenu wazoefu na kilimo pia watu wengine.