Naomba ushauri: Nimechoka kusoma nataka kumiliki biashara yangu

J boaz

Member
Joined
Sep 26, 2019
Posts
15
Reaction score
7
Mimi ni mwanafunzi ambae namalizia elimu yangu ya biashara CBE ila kwa sasa siitaji tena kuendelea na masomo naitaji kuanzish biashara yangu binafsi na biashala ninayo taka kufanya ni biashara ya kuuza nguo za mtumba za kike japo sio mala ya kwanza kufanya hii biashara ila kwa sasa nataka niifanye kwa malengo zaidi ata kufungua branch tofauti tofauti ila paka sas nina mtaji wa laki5 ambapo nimesha nunua baadhi ya vifaa vya dukani kama midoli henga, stend ya nguo nk lengo ni kuongeza thamani katika biashara hiii na kuifanya kitofauti zaidi.

Kwa kipind cha nyuma nilikuw nauwezo wa kununua mzigo wa laki na nusu na kupata faida adi laki na30.

Nanunua jeans nzuri kwa elfu3 nauza kwa elf8 adi elfu 10 kilingana na mteja ninaye muuzia top nanunua kwa elf moja na kuuza elfu 4, gauni fupi haswa za kutokea usiku nanunua kwa elf3 au elf2 nauza kwa elf8 adi elf10.

Ukiangalia nibiashara yenye faida kwa kiasi chake ila apo sikuwa na duka maalumu nilikuwa nawauzia2 wanafunzi wenzangu kwa sas nataka nichukue frame japo sijapat bado na location ya biashara ila target yangu ni wanafunzi wa chuo na baadhi ya watu around.

Naomba ushauri kwa wenye uzoefu wa biashara nawezaje ku manage biashara yangu bila kupata hasara pia njia gani naweza kutumia ili kukuza biashara yangu ya mitumba.
 
Mimi ningekushauri umalize chuo brother!!! Kama ada ipo hudaiwi, huna vimeo (sup na carry) vya kukukwamisha ni vyema ukamaliza masomo yako ukapata cheti chako then mambo mengine yatafata.

Usishawishike na hizo faida ukasahau kilichokupeleka chuo ukajikuta unashindwa kufikia malengo!! Chuo yenyewe sidhani kama ni zaidi ya miaka 3 muda mfupi sana ni heri umalize masomo kwanza!

Japo ajira ni ngumu lakini cheti muhimu, ni moja ya silaha huku mtaani hasa kama hiyo mipango ya biashara itakwama na huna pa kutokea tena!!

Binafsi nilivyokuwa chuo nilikuw na mshkaji wangu tulipiga sana biashara vijijini huko tukawa tunalaza faida ya kutosha tu per day, mwenzang akaacha hadi chuo akaendelea nayo akawekeza huko karibia 3M+ ila leo hii biashara ishakufa na masomo hakumaliza yupo anapambana tu mtaani, sometimes namwambiaga at least hata ungekuwa na gamba lako la kuzugia tu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada, nilishakuwa na rafiki, alikuwa na kipaji cha kucheza tennis, Baba yake alikuwa engineer. Kama walivyo Waafrika wengi mzee aliamini hakuna maisha bila elimu.

Jumamosi rafiki yangu alikuwa na tuition ya maths na science wakati wenzake wana practice tennis. Alikuja kwenda university kusoma Pharmacy degree.

Sasa hivi Baba yake ni marehemu, yeye ni Pharmacist mkubwa tu na tennis anacheza kama hobby Gymkhana weekends. Anamshukuru sana baba yake kila siku.

Back to your point, maliza shule uwe na Cheti, biashara fanya kama hobby. Ikibuma cheti chako kinaweza kukukomboa.
 
Usiache chuo. Kama tayari mtaji unao na baadhi ya nyenzo za kuanzia na biashara una uzoefu nayo mimi nakushauri soma huku unafanya biashara yako. Hapo ni suala la kubalance muda wako kwenye masomo na biashara.

Mfano kama chuoni kwasasa unasoma morning session unaweza kuhamia evening session ili mchana ufanye biashara yako kisha jioni uingie darasani. Ukiwa na nia na malengo utafanikiwa. All the best mkuu.
 
Kama wateja wako ni waachuo nakusihi endelea kuwauzia hvyo hvyo.Mara nyingi hizi frame mzee hakuna maslahi utaita tra na kodi ya pango bure.
Endelea kuzungusha hvyo mpaka mtaji ùkue vya kutosha ndipo wazo la frame lije baadae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakusema anataka kuacha chuo.

Portfolio | 2020
 

Well said..super woman..!!!
 
Watanzania wanapenda kukurupuka kujibu kabla hawajaelewa!ni wapi mtoa mada kasema anataka kuacha shule????kweli humu kuna vilaza zaidi ya Fb


Sent using IPhone X
 
Savage94 nashukuru sana kwa ushauri wako naanza kuona umuimu wa kuendelea na masomo
 
Kulingana na matatiz ya kifamilia naona kuna Haja ya kufany biashara angalau niweze kusaidia japo kwa kiasi chake bat at the same time naona umuimu wa kuendelea na chuo what should I do
 
Thanks brother naomba nifanyie kazi kwa ulicho nambia
 
Ukiwa unatembez faida inaonekan bat mda mwingine unapo ongea na baadhi ya wateja wanauliza permanent prace ambayo napatikana na Lengo ni kukuza biashara na brand at the same time
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…