Naomba ushauri, nimezoea kuendesha automatic sasa juzi nimepata manual Vitz

Rosati

Senior Member
Joined
Feb 9, 2013
Posts
104
Reaction score
69
Naomba ushauri, nimezoea kuendesha automatic sasa juzi nimepata manual Vitz.
Kila nikisimama kwenye foleni hapa dsm foleni ikiachia gari inazima, nilidhani ni technical problem lakini fundi akaniambia sio problem.
Hivi tatizo ni nini inazima nikiwa nataka kuondoka baada ya kusimama kwenye foleni.
Ni kilometer au mwendo kiasi gani ili niweze kubadilisha gear.
 
Inabidi ujifunze kuendesha gari za 'manual transimssion'

Tafuta dereva anayejua akuelekeze kwa vitendo ukiwa na gari.

Ama nenda shule ya udereva japo kwa wiki moja kufanya refresher course.

Kwa maelezo tu ya maandishi unaweza usiambulie kitu ama kuelewa tofauti kabisa kwakuwa kujieleza na kutafsiri maandishi ni kipaji pia.

Pia waweza ingia youtube na kutafuta "how to shift in manual gearbox"
 
Shukran mkuu
 
Dah...nakatamani hako. Ukizoea manual auto sijui unaionaje. Haswa upate manual ambayo unaunguruma uta enjoy ww na abiria wako na audience zile kuvesha na kuvua. Acha kabisa. Tupe picha ya hiyo vits boss. Natamani ist manual alafu dash body ikae usawa wa dereva sio katikati kama ilivyo sasa. Nikotayari kukuelekeza nini chakufanya isizime.



Mungu wetu sote.
 
Nieleze mkuu
 
Hiyo Gari Unatakiwa Muda Wote Kuondokea Gear Number 1,Mambo Ya Number Mbili Labda Ingekuwa Gari Inayotumia Diesel
Shida ipo pale kwny kuachia clutch afu kurudisha mguu kwny wese hapo ndipo uchawi ulipo kubalansi mambo...

Mie nilijufunza driving ten years ago ila sijagusa tena manual ila ninachojua manual uchawi wale upo kwny kuondoka tu ikishashika mwendo haina tofauti na auto...

Mtoa mada usiombee ukute folen ya kilimani afu wa nyuma yako kaa zero distance huwa patamu hapo
 
Hii scenario imenikuta sana pale kwenye kamwinuko pale kutoka rafia kuelekea tegeta kwenye mataa ya mbuyuni. Kelele nlizopigiwa pale mpaka nikazima gari na kuwasha hazard.

Hapo kwenye kuswitch clutch na mafuta ndio panapochanganya yaan
 
Hii scenario imenikuta sana pale kwenye kamwinuko pale kutoka rafia kuelekea tegeta kwenye mataa ya mbuyuni. Kelele nlizopigiwa pale mpaka nikazima gari na kuwasha hazard.

Hapo kwenye kuswitch clutch na mafuta ndio panapochanganya yaan
Ukiweza hapo umeweza manual nenda barabara zisizo bize hadi uzoee usije kula buyu huko njia kubwa
 
Ka -adjust krachi yako,
 
Clutch pedal huwa imejikunja kurudi juu!

Unapoiachia usiinue mguu kuifuata bali iachie kwa kurudisha mguu nyuma ukihakikisha kisigino chako hakitengani na floor ya gari.

Pia fanya mazoezi kwenda mbele na kurudi nyuma sehemu za wazi mara nyingi uwezavyo. Hii itakusaidia kujua clutch yako inaruhusu gari kutoka ikiwa level ipi chini, katikati au juu.

Kama ili gari itoke clutch inakulazimisha kuiachia mpaka juu, ita fundi ai'adjust' ili ukilegeza tu mguu ianze kuondoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mdau umenifungua macho. Ahsnate sana. Nahisi nimepata suluhisho la tatizo langu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…