LD
JF-Expert Member
- Aug 19, 2010
- 3,014
- 578
asante kwa maneno yako mazuri nayaheshimu. sikuwa na nafasi ya kusema kila kitu hapa maana ningechukua nafasi kubwa hata kusoma ungeshindwa.
lakini nimetoa mfano mmoja tu wa mambo anayonifanyia huyo mpenzi wangu wa awali, lakini kuna mengi ikiwa ni pamoja na hata kufukia kuwa na uhusiano wa kimapenzi na rafiki yangu na niligundua hilo na akaomba radhi.
yako mengi lakini pamoja na yote hayo bado nimekuwa mvumilivu mwaka wa sita huu hadi ninapoona kama huko tunakoelekea si shwari na umri wa kuoa unazidi kuyoyoma ndipo nikaona niangalia upande mwingine.
Nimeshakaa naye several times na kuongea naye, tuki-solve kitu leo, after sometime kinarejea upya hadi najikuta nachoka. hadi kufikia kuanzisha uhusiano mpya nimevumilia mengi sanaa toka kwake lakini nimefikia kukata tamaa
Ni kweli unaweza ukaongea mengi hapa. Lakini natamani tungepata neema ya kumsikiliza na huyo dada pia. Yani hakuna kujihesabia haki hapa. Kama uliona hakufai, ilikuwa ni swala la kumtangazia kuwa hakufai na humpendi na umechoka kuvumilia.
Na unakwenda kuanza mahusiano na mtu mwingine, lakini kama nimekusoma nikakuelewa ni kwamba unawachanganya wote wawili. Ahii kwani umeambia ni Maharage na ubwabwa hata uvichanganye pamoja?
Kwa kweli sipendi maamuzi ya hivi. Huna msimamo kaka unacheza pata potea na maisha ya wadada wa watu?