Naomba ushauri tiba asili ya tonsils maana hospitali nimefeli kupata dawa ya kudumu

Kuna dawa moja ya kimasai siijui jina ila ya unga unasuguriwa nayo kwenye koo asubuhi kabla hujala chochote inauma Ila inasaidia sana
 
Salaam.
Wadau wa JF, nna Mdogo Ang wa myaka 17 anateseka Sana na shida ya tonsils.

Ametibiwa hospitali Mara kadhaa, Hasa akiwa anakaa shule Ila shida imebakia kuwa nzito akahamia day.

From there tatizo limepungua Ila humrudia Kila Mara Licha ya kutumia doze na kumaliza.

Kila akila kitu Cha baridi Kama matunda, maji ya kunywa, mkate au chochote ambacho hakifuki mvuke saa za jioni au hata mchana ikiwa hakuna jua kali basi kesho na keshokutwa yake dogo ni mgonjwa na ni mgonjwa Haswa.

Msaada wenu tafadhari ikiwa Kuna anayefahamu tiba ASILI ya tatizo Hilo au ushauri zaidi kulingana na experience .
Matibabu ni ya aina mbili
1)Ampicloxaccilin or pen V
2)operation chaguo ni lako
 
Hizo tonsils zinisumbua niko mdogo sjui darasa la kwanza, sikumbuki vizuri nami zilikuwa zikinisumbua ivo ivo dawa za kienyeji za kula nlipewa, kwa wachina nlienda ila holaaa nliangaika nazo miaka nafikiri 5 nikajaga kufanyiwa upasuaji niko std vi wakazitoa enzi za September eleven ya Osama 😃😃 ilikuwa pale KCMC since siku hizo sijawahi kupata shida mabarafu natafuna mpaka leo.
 
Salaam.
Wadau wa JF, nna Mdogo Ang wa myaka 17 anateseka Sana na shida ya tonsils.

Ametibiwa hospitali Mara kadhaa, Hasa akiwa anakaa shule Ila shida imebakia kuwa nzito akahamia day.

From there tatizo limepungua Ila humrudia Kila Mara Licha ya kutumia doze na kumaliza.

Kila akila kitu Cha baridi Kama matunda, maji ya kunywa, mkate au chochote ambacho hakifuki mvuke saa za jioni au hata mchana ikiwa hakuna jua kali basi kesho na keshokutwa yake dogo ni mgonjwa na ni mgonjwa Haswa.

Msaada wenu tafadhari ikiwa Kuna anayefahamu tiba ASILI ya tatizo Hilo au ushauri zaidi kulingana na experience .
Nenda hospital zilizospecialize kwa ENT watampima kama ni kuzitoa (tonsillectomy) watakwambia, na zikitolewa utaishi kwa raha sana bila maudhi
 
Back
Top Bottom