Naomba ushauri: ukifiwa, unavukaje maumivu na kusonga mbele na maisha?

Naomba ushauri: ukifiwa, unavukaje maumivu na kusonga mbele na maisha?

Hamna cha kufanya, muda ndo tabibu wa majonzi.

Japo juhudi zozote zinazoonesha kujali haziharibu chochote,

Ila ni lazima aumie, hamuwezi kufuta kumbukumbu.
 
Pole yake sana,hakika ni jambo gumu na la kuumiza haina kifani jamani kufiwa na mtu wa karibu yako,mimi hapa nilifiwa na classmate wangu pascal mpaka leo nashindwa kuelewa kwa nini duniani tupo,nina kovu moyoni. Sembuse wazazi,jambo hili lisikie kwa jirani. Mungu awatie nguvu wote waliofiwa na wapendwa wao wawapendao.
 
Rafiki yangu amefiwa na mama mzazi na mdogo wake siku moja kwenye ajali. Anaumia sana, imepita wiki sasa, ila bado analia kila siku na kuongea peke yake mpaka tunaogopa.

Kama umeshawahi kufiwa na mtu wa karibu, nini kilikusaidia kutuliza maumivu na kuweza kusonga mbele?


View attachment 3220933
muache alie tu na kama n mtumiaji wa vinywaji mchangamshe hata na bia 4 za baridi.
 
Muunganisheni na wataalam wa afya akili. Nao wanasaidia sana. Pia awe karibu sana na M/Mungu.
 
Muda ndo kila kitu she will be fine as the time passes.
Namimi niltaka ni comment ivo

Muda ndo unaponya maumivu yoyote makali life must goes on wengine tulishapita hayo but kuondokewa na mpendwa wako kunaumiza sana ila sio mwisho maisha yako.
 
kila kitu kitajichuja taratibu miezi 6 mbeLe....

ONYO ,mwambie miezi 6 ipite bila kupigwa miti.....akipigwa tu yatakayomkuta asinitafute
 
Pole yake sana. Muache alie,machozi ni tiba ila tu msimuache peke yake kwa muda mrefu kaeni nae karibu na shughuli za hapa na pale,kutembea tembea na kusikiliza vipindi vya dini vitamsaidia sana.
 
Back
Top Bottom