Mkuu kama huna experiance ya biashara na hujui nini ufanye na 50 zako, ni too risky kuinject hiyo pesa kama muanzaji. Nakushauri utakapopata idea ya nini cha kufanya anza taratibu na mtaji mdogo kidogo ya huo, kama 10-15m kwa kuanzia, hii itakusaidia kuwa na back up ya kutosha kukabiliana na contingencies za kibiashara. Jipe muda wa kugrow taratibu, ndani ya mwaka utakuwa na uzoefu wa kutosha na utakuwa umeshajifunza mengi sana.
Siri kubwa ya biashara si idadi ya pesa mingi utakazoingiza kama mtaji au katika mzunguko. Siri ni kuwa na muda wa kutosha kusimamia biashara yako, kujifunza zaidi na zaidi kila siku. Na kujituma pamoja na kujifunza kutoka kwa wengine...
Kama utasisitiza kuanza na 50m, Binafsi ningekushauri ununue tractor unit moja na trailer yake kutoka UK, wakati ipo njiani anza mchakato wa kukuza mtandao wako na wafanya biashara hiyo. Utajifunza mengi ndani ya mwezi na utakuwa tayari kuifanya gari itakapofika. Ukiwa na bima salama, na dereva mwerevu na mweledi, ndani ya mwaka utakuwa umesharudisha hela yako. Na unaweza ukawa na mawili ndani ya miezi 10, hii ni pale tu utakapokuwa na adabu na fedha (usifanye matumizi holela ya mapato yanayotokana na gari). Na kama uko tayari, safiri nalo gari lako. Anza na mbao mafinga to dar, trip 1 ni 2.5m, kwa mwezi unaweza kupiga hizi kama 7 kama uko serious.
Karibu.