kyanyangwe
JF-Expert Member
- Oct 31, 2018
- 1,275
- 3,316
Kuna sehemu nilipata kazi private sector sasa yapata mwezi mmoja umepita,mkataba nilisaini sehemu yangu ile ya employee ila employer hakua amesaini,nikamkabidhi HR wa kampuni na taratibu nyingine za kuwa on borded zikafuatwa.sasa mpaka Leo hr hajanipa copy ya mkataba wangu ambayo imesainiwa na pande zote mbili(mwajiri na mwajiriwa) nikajaribu kuuliza kwa staff wenzangu wakongwe hapa kazini wakaniambia ndo kawaida ya hii kampuni huwa hawatoi copy za mikataba kwa staff wao kwa sababu eti kufukuzwa ni nje nje hivyo wao wanajihami na mambo ya CMA.so baada ya kuangalia mazingira ya kazi yalivyo nikajiona kama mimi ni kibarua tu hapa hivyo nimepanga nikishachukua mshahara wangu wa mwezi huu nisepe bila hata kuaga.
Je hii kisheria imekaaaje wakuu?
Je hii kisheria imekaaaje wakuu?