Naomba ushauri wa kisheria kama sitazulumika katika mauziano haya ya nyumba

Naomba ushauri wa kisheria kama sitazulumika katika mauziano haya ya nyumba

Yaani mmefikia hatua hamuaminiani kiasi hiki?

Mmeshaenda mahakamani kila kitu kipo kisheria kwanini bado mnaogopa? Wekeni sahihi mchukue hela nyie watu.

Hata ingekluwa mimi nisingewapa hela hadi msaini. Nyumba za urithi ki kasheshe sana, unanunua leo kesho unaitwa mahakamani ndugu wengine wamefungua kesi. Ikiwa nyinyi mmeshakubaliana sioni kwanini hamuiamini mpaka mahakama. Uzuri mmefuata hatua zote. Mkisaini na asipoweka hela si mnarudi mahakamani kumshtaki?
Mirathi achana nayo kabisa.

Wasipogombama watoto ndg upande wa mama au. Baba
 
Mnaweza mka saini huo mkataba mkauacha mahakamani/hakimu kisha mkaongozana na mnunuzi hadi benki kuhakikisha amelipa. Baada ya kulipa kwa wote ndio anakabidhiwa mkataba.

Hao majamaa wapumbavu tu.

Hata wasipouacha mahakamani.

Valid Deposit slip bila kuletwa mahakamani ama kwa mwanasheria.. mkataba unakuwa void
 
Msimamizi wa mirathi ndie anaepaswa kuuza nyumba hiyo
Msimamizi wa mirathi hajui afanyalo.

shida tuliyo nayo Msimamizi wa Mirathi akishateuliwa huwa hapewi legal instructions za sheria inamtaka afanye nini.

Unategemea raia wa kawaida akasome Probate and Administration Of Estates Act pamoja na Indian Succession Law of 1865 pamoja na Land Act na Land Registration Act akazielewa? Impossible.

Kwa saab hata pedestrian lawyers wengi hawazielewi, wanasheria 8 kati ya 10 hawazielewi, na wakizielewa hawazifuatishi! Including resident magistrates and high court judges! It is pathetic.

Unauziwaje mali ya urithi na watoto wakati mirathi imepitia mahakamani ????
 
Kuna nyumba ya urithi,wanafamilia wahusika wote tumekubaliana kuiuza,na tumeandika muhtasari wa kikao cha kuuza,kiasi cha pesa na mgawanyo wake wote,tumeukabidhi mahakamani.

Jambo linalotutatiza ni jinsi ya kulipana,
Mnunuzi anasema tusaini makubaliano ya kuuziana ndipo aweke pesa kwenye bank account zetu.
Lakini baadhi yetu wanasema kusaini ni mpka pesa iingie kwenye account zao

Mauziano yanafanyika mbele ya wakili wa mahakama kuu,

Biashara inataka kushindikana kutokana na huu mvutano.

Pia hakimu mwenye faili letu alisema faili halifungwi mpaka tutakapopeleka ushahidi wa malipo halali kwenye account zetu ndio atalifunga

Naomba ushauri je Kipi kianze ili kunusuru huu mkwamo?

Ipo hivi mkuu

Anayeuza nyumba kwa niaba yenu ni msimamizi wa mirathi na sio familia nzima mmoja mmoja(muktasari wa kikao ndio ridhaa yenu kisheria)

Anachotakiwa kufanya msimamizi ni kuchukua muktasari wa makubaliano yenu ya kuuza nyumba na makubaliano ya kila mtu atapata mgao kiasi gani pamoja na makubaliano ya mnunuzi atalipa kiasi gani
Then msimamizi ataandika barua kuomba mahakama imtake mnunuzi kufika mahakamani kukamilisha manunuzi

Mahakama itaandika barua kumuelekeza mnunuzi kuingiza hela kwenye acc maalum ya mirathi ya mahakama kisha aje mahakamani na risiti ya malipo kwaajili ya kuja kusaini na kukabidhiana hati za nyumba na msimamizi

Kuanzia hapo sasa kila mrithi atapeleka acc no yake mahakamani na ataingiziwa mgao wake kulingana na makubaliano yenu
Au kila mmoja ataandikiwa cheki yake kwa mujibu wa mgawanyo

Vinginevyo mtoke wote na mnunuzi wenu muende mahakamani, msimamizi atamalizana na mnunuzi amkabithi mzigo oalepale cash mahakamani kisha karani wa mahakama ataanza kuwagawia kila mmoja na mzigo wake
 
(muktasari wa kikao ndio ridhaa yenu kisheria)

Kikao ndio ridhaa ya kisheria ?

Kwa hiyo ukihudhuria kikao ukazimwa by tyranny of the majority huwezi kuja pinga maamuzi ya kikao ?

Kuna sababu kwa nn neno kikao hulikuti kwenye sheria.

Hebu taja sheria yeyote ile ya inayotamka maneno "muhtasari wa kikao cha familia / wanandugu / ukoo / warithi )" kwenye shauri la mirathi.
 
Kikao ndio ridhaa ya kisheria ?

Kwa hiyo ukihudhuria kikao ukazimwa by tyranny of the majority huwezi kuja pinga maamuzi ya kikao ?

Kuna sababu kwa nn neno kikao hulikuti kwenye sheria.

Hebu taja sheria yeyote ile ya inayotamka maneno "muhtasari wa kikao cha familia / wanandugu / ukoo / warithi )" kwenye shauri la mirathi.
Mimi sio mwanasheria ila nimesimamia mirathi

Mkuu ikiwa yatatakiwa maamuzi ya watu zaidi ya mmoja sheria itatambua maamuzi yao iwapo tu wataandika makubaliano yao na kila mmoja ata tia saini kukubaliana na maamuzi hayo
You may call it whatever ila kwenye mirathi unaitwa MUKTASARI WA KIKAO CHA FAMILIA/UKOO/NDUGU
Ni kikao cha familia tu ndio chenye MANDATE ya kuteua msimamizi wa mirathi

Iwapo kwenye kikao cha familia mtashindwa kuafikiana basi mahakama itaamua

Mswala ya mirathi kwanza kabisa huwa wanaachiwa wanandugu wagawane kwa mujibu watakavyo ona inawafaa LAKINI wanapo shindwa kukubaliana basi mahakama itakwenda kuamua kwa mujibu wa sheria kama ni ya kiislam au kimila au kiserikali

Kwenye shauri la mirathi MUKTASARI WA KIKAO CHA UKOO ni document muhimu kweli na hakifanyiki kitu chochote bila hiyo
 
Kwenye mkataba wekeni kipengele kinachosema kuwa makubaliano hayo yatachukuliwa kuwa yamekamilika pale fedha zitakapokuwa zimeingia kwenye akaunti ya kila mhusika. Wekeni saini zenu. Ikiwezekana na akaunti hizo zitajwe kwenye hayo makubaliano.
 
Hakuna atatizo, ndio ni sawa mnasaini, kisha mnakabidhi documents wakili wa mahakama kuu mnayemtumia,

Na wakili wa mahakama kuu anasubiri uthibitisho wa 1. mnunuzi; 2. wauzaji (kuwa tayari fedha imepokelewa) ili kufunga faili na mauziano yatakuwa yamekamilika.

Hivyo nyote | mnunuzi na wauzaji , wakili wa mahakama kuu ndiye anawasimamia
Ndivyyo tulivyokubaliana kila mmoja apokelee pesa kwenye account yake,kadhalika msimamizi hilo kakubaliana nalo na mnunuzi pia kakubali kufanya hivyo
Issue hapa tukisaini ndipo aweke pesa iko sawa?
Ila hakikisha kwanza huo mvutano; wa kipi kitangulie Pesa au Saini; wakili wenu anatambua kwanza ndipo muendelee baada ya kushauriana naye na kufikia muafaka wa kusaini kwanza then malipo ndio yafuate. Hapo wote mko salama.
 
Hili la mirathi ni kubwa sana kwa matajiri Kenya. Kuna familia za matajiri kesi za mirathi zimefikia mpaka miaka ishirini na hazijaisha (mapingamizi, rufaa nk), mawakili tu ndiyo wanafaidi.
 
Yaani mmefikia hatua hamuaminiani kiasi hiki?

Mmeshaenda mahakamani kila kitu kipo kisheria kwanini bado mnaogopa? Wekeni sahihi mchukue hela nyie watu.

Hata ingekuwa mimi nisingewapa hela hadi msaini. Nyumba za urithi ni kasheshe sana, unanunua leo kesho unaitwa mahakamani ndugu wengine wamefungua kesi. Ikiwa nyinyi mmeshakubaliana sioni kwanini hamuiamini mpaka mahakama. Uzuri mmefuata hatua zote. Mkisaini na asipoweka hela si mnarudi mahakamani kumshtaki?
Shukrani kwa ushauri wako
 
Hili la mirathi ni kubwa sana kwa matajiri Kenya. Kuna familia za matajiri kesi za mirathi zimefikia mpaka miaka ishirini na hazijaisha (mapingamizi, rufaa nk), mawakili tu ndiyo wanafaidi.
Nomaa
 
Mnaweza mka saini huo mkataba mkauacha mahakamani/hakimu kisha mkaongozana na mnunuzi hadi benki kuhakikisha amelipa. Baada ya kulipa kwa wote ndio anakabidhiwa mkataba.
Shukrani kwa ushauri wako
 
Back
Top Bottom