Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Neo-Christianity hiyoAcha ujinga mkuu hakuna mkristo anae owa wanawake wawili mke halali ni mmoja tuu hao wengine ni masuria tu, pia uwe unasoma ulicho andika kabla ya kuposti
Kwa kuongezea tunaweza kataa ukweli lakini hatuwezi epuka matokeo yatokanayo na ukweli! Mwanaume aliyekamili ni wachache wenye kutosheka na mmojaMimi ni mkristo lakini nikiisoma Biblia hua naielewa vizuri kwamba mwanaume kua na wake wengi siyo dhambi, au kuna mtu anaekijua kifungu cha kwenye Biblia kilichoandikwa kuoa wake zaidi ya mmoja ni dhambi akilete hapa watu tujifunze.
45 years man with 10 children! Ongeza mmoja utimize timu ya mpira!Mimi ni Mwanaume mwenye umri wa miaka 45, ni Mkristo dhehebu KKKT, mwaka 2001 nilifunga ndoa ya Kikristo na nimefanikiwa kuwa na watoto 5, mwaka 2007 kulikuwa na mgogoro mkubwa katika ndoa uliopelekea kutengana kwa muda wa mwaka mmoja
Wakati huo tulikuwa na watoto 2, wakati tumetengana nilikutana na mwanamke mwingine na nilimpa mimba, lakini alienda chuo akiwa na mimba mbali na mimi, niliendelea kumpa matunzo akiwa chuoni lakini mke wangu naye alijirudi na tukaendelea na maisha
Hivyo nikawa naishi na wake wawili lakini bi mkubwa hakuju, niliendelea na maisha hayo lakini katika wakati mgumu, bahati nzuri nilienda chuo kusoma na huko nako nikazaa na mwananke mwingine, kwa ufupi hao wote naishi nao na wanafahamiana
Bi mkubwa sasa ana watoto 5 wawili wa kike na wakiume 3, mke wa pili ana watoto wawili wote wa kiume, bi mdogo ana watoto 3 wawili wa kiume na wakike mmoja, nimetoa mahari kwa mke wa pili na bi mdogo, wote ni wakristo, bi mkubwa nimeishi naye miaka 18 sasa
Mke wapili nina miaka 11 na bi mdogo miaka 7, kila mmoja ana kwake na nina mashamba kadhaa na viwanja mbalimbali, je sheria inasemaje kuhusu khaki ya kurithi mali, nikiwa hai au nikiwa nimekufa kwa bahati mbaya, naomba sana mnishauri kisheria zaidi
ahsanteni