Naomba ushauri wa kisheria kuhusu Vodacom Mpesa

kambagasa

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2014
Posts
2,269
Reaction score
1,803
Ndugu zangu sikutaka kuleta huu uzi kama mfanyabiashara mdogo kuomba msaada wa kisheria kuhusu kampuni ya Vodacom Tanzania.

Ninavyoandika huu uzi ni mwezi sasa nilituma pesa kwenda akaunti yangu kama akiba ili nitakapofikia kiasi ninachotaka kinisaidie katika manunuzi ya bidhaa.

Tangu siku natuma nilipokea tu sms yao Vodacom hivyo nikasubiri sms ya bank ambayo sikuipata.

Baada ya masaa machache nilipiga Vodacom Mpesa wakaniambia pesa yangu haijaenda bank na iko 'hewani" hivyo nisubiri masaa 24.

Masaa hayo yakapita nikapiga simu tena na kupewa siku kumi za kazi watakuwa wameshanirekebishia aidha wazirudishe ama ziende bank.

Ndugu zangu ninavyoandika hapa nishapiga simu zaidi ya 20 hapo Vodacom huduma kwa wateja lakini majibu yao ni tunashughulikia.

Baadae nikaamua kwenda Voda shop mjini huko nikaambiwa nitoe kopi ya kitambulisho na nikapewa masaa 24 hata hivyo hadi leo pesa haipo bank wala haijarejeshwa kwenye namba yangu ya Vodacom (akaunti yangu ya Mpesa).

Siku tatu zilizopita nilipiga simu hapo Vodacom akapokea kaka mmoja ambaye alinijibu kwa hasira na dharau kuwa maadamu ulipata meseji ya muamala Vodacom hatuhusiki hivyo nenda bank ukaangalie pesa yako.

Nilimwambia siku hiyo niliangalia pesa bank na haijafika hata hivyo kuna mfanyakazi hapo bank huwa ananisaidia sana kila nikihitaji kufahamu kama pesa ishaingia pia kupitia simu yangu ambayo imesajiliwa kupata taarifa mbalimbali za akaunti yangu.

Baada ya majibu ya huyo kaka nilipiga tena akapokea dada mmoja ambaye namshukru alinieleza kwa kina kuwa wao wakipokea pesa huwa wanazituma kwa vendor (kati ya shivacom sinauhakika) baadae ndipo zinaenda bank lkn wamekuwa wanatoa hizi taarifa hapo kwa vendor lkn hatoi mrejesho (anakaa kimya).

Ndugu zangu ni hatua zipi nichukue ili
(1) Nipate pesa zangu?

(2) Gharama na muda wa kufuatilia pesa zangu?

Tashukuru sana ndugu zangu ukizigatia pesa kwa wakati huu ni ngumu sana kuipata leo hii iko haijulikani ilipo.

NB: Niko tayari kutoa kumbukumbuku za huo muamala pm kwa atakayetaka kuhakiki.
 
Pole boss Mimi mwenyewe nililipia pesa NACTE lkn mpaka leo sikupewa code zozote na pesa haikurudi
 
Ya kwangu hata sitaki kuyasema kwa kua yalishapita,ila kiukweli wanasumbua sana,na mala kadhaa wanakua na majibu hayafanani na hayana matokeo mazuli
 
Ya kwangu hata sitaki kuyasema kwa kua yalishapita,ila kiukweli wanasumbua sana,na mala kadhaa wanakua na majibu hayafanani na hayana matokeo mazuli
Fikiria umbali wa kilometa 75 hadi Voda shop harafu hadi leo pesa haijulikani kama itarejeshwa.
 
Hakuna utaratibu wa kisheria kwa hawa watu?
Yamkini ikawepo japo sijawah kufanya hvyo sina majibu ya uhakika,mimi walikaa na laki mbili na thelasini zangu mwezi mzima na kidogo mpaka nikatamani niikate kate line yao
 
ushauri wangu kwa jamii ni kwamba hizi huduma za kutoa pesa bank kwenda kwenye mitandao ya simu na kutoa pesa mitandao ya simu kwenda bank na kutuma pesa mtandao wa simu moja kwenda mtandao wa simu mwingine hizi huduma haziko sawasawa kwenye mifumo yao na ndio maana kila siku malalamiko ya watu kupoteza pesa na muda

kifupi hizi huduma hawajajipanga wote kikamilifu ni heri kuishi kama enzi za ujima tu ili pesa zako ziwe salama kama ni kwenda kwenye ATM ni bora kwenda kutoa pesa na kama ni mitandao ya simu basi uwe huohuo

majirani zetu hapo wanaongoza kwa miamala ya simu ila hawana changamoto kama zetu hapa

hizi huduma kwetu ni bahati nasibu au karata tatu màana ukiwa unataka kufanya roho inakuwa juu na yakishakukuta utajuta..
 

Mimi Yalinikuta kama ya kwako, nimehangaika nao wee wala hela yangu haikurudishwa, niliamua kuachana nao,
Kisheria unaweza kuwashtaki tatizo "terms and conditiona apply" Wewe unachotakiwa kuangalia ni cost utakayotumia kuwafuatilia in terms of money, time and brain then take your decision.
 
Nenda TCRA, wao watafuata kuona kuna nini. Somebody Mungi can help
 
Mungu akubariki sana ndugu. Ngoja niwatafute
Bonyeza hapo pa complaint, itakuja website ya TCRA, then nenda kwenye kiswahili, jieleze tuma. Nitakutafutia namba za Mungi nilikuwa nazo umpigie,. Ni Mkurugenzi wa mawasiliano na huduma za wateja
 
Bonyeza hapo pa complaint, itakuja website ya TCRA, then nenda kwenye kiswahili, jieleze tuma. Nitakutafutia namba za Mungi nilikuwa nazo umpigie,. Ni Mkurugenzi wa mawasiliano na huduma za wateja
Tashukru sana
 
Online complaint form- kuna ya kiswahili.

0784558270 - 1 jaribu namba hiyo pia mapokezi waeleze shida yako may be watakupa guidance.
Asante sana. Ngoja niwape maelezo yote then niwapigie
 
Malalamiko yote juu ya uendeshaji wa mitandao ya simu huanzia TCRA. Jaza complain forms zilizo katika website ya TCRA hapo utasaidiwa

Pia jedwali hilo litakusaidia.
 
Malalamiko yote juu ya uendeshaji wa mitandao ya simu huanzia TCRA. Jaza complain forms zilizo katika website ya TCRA hapo utasaidiwa

Pia jedwali hilo litakusaidia.
Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…