kambagasa
JF-Expert Member
- Aug 18, 2014
- 2,269
- 1,803
Ndugu zangu sikutaka kuleta huu uzi kama mfanyabiashara mdogo kuomba msaada wa kisheria kuhusu kampuni ya Vodacom Tanzania.
Ninavyoandika huu uzi ni mwezi sasa nilituma pesa kwenda akaunti yangu kama akiba ili nitakapofikia kiasi ninachotaka kinisaidie katika manunuzi ya bidhaa.
Tangu siku natuma nilipokea tu sms yao Vodacom hivyo nikasubiri sms ya bank ambayo sikuipata.
Baada ya masaa machache nilipiga Vodacom Mpesa wakaniambia pesa yangu haijaenda bank na iko 'hewani" hivyo nisubiri masaa 24.
Masaa hayo yakapita nikapiga simu tena na kupewa siku kumi za kazi watakuwa wameshanirekebishia aidha wazirudishe ama ziende bank.
Ndugu zangu ninavyoandika hapa nishapiga simu zaidi ya 20 hapo Vodacom huduma kwa wateja lakini majibu yao ni tunashughulikia.
Baadae nikaamua kwenda Voda shop mjini huko nikaambiwa nitoe kopi ya kitambulisho na nikapewa masaa 24 hata hivyo hadi leo pesa haipo bank wala haijarejeshwa kwenye namba yangu ya Vodacom (akaunti yangu ya Mpesa).
Siku tatu zilizopita nilipiga simu hapo Vodacom akapokea kaka mmoja ambaye alinijibu kwa hasira na dharau kuwa maadamu ulipata meseji ya muamala Vodacom hatuhusiki hivyo nenda bank ukaangalie pesa yako.
Nilimwambia siku hiyo niliangalia pesa bank na haijafika hata hivyo kuna mfanyakazi hapo bank huwa ananisaidia sana kila nikihitaji kufahamu kama pesa ishaingia pia kupitia simu yangu ambayo imesajiliwa kupata taarifa mbalimbali za akaunti yangu.
Baada ya majibu ya huyo kaka nilipiga tena akapokea dada mmoja ambaye namshukru alinieleza kwa kina kuwa wao wakipokea pesa huwa wanazituma kwa vendor (kati ya shivacom sinauhakika) baadae ndipo zinaenda bank lkn wamekuwa wanatoa hizi taarifa hapo kwa vendor lkn hatoi mrejesho (anakaa kimya).
Ndugu zangu ni hatua zipi nichukue ili
(1) Nipate pesa zangu?
(2) Gharama na muda wa kufuatilia pesa zangu?
Tashukuru sana ndugu zangu ukizigatia pesa kwa wakati huu ni ngumu sana kuipata leo hii iko haijulikani ilipo.
NB: Niko tayari kutoa kumbukumbuku za huo muamala pm kwa atakayetaka kuhakiki.