Naomba ushauri wa kisheria

Anold

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2010
Posts
1,456
Reaction score
615
Baada ya kuona tangazo la kazi gazetini rafiki yangu aliandika barua na kuomba kazi hiyo kama maelekezo yalivyotaka. baadaye aliitwa kwenye usaili wa kwanza akafanikiwa kupita kwani waliomba zaidi ya watu 50, waliobaki walikuwa 15 ambapo walifanyiwa usaili tena wa kujieleza ambapo rafiki yangu huyo alifanikiwa kupata nafasi hiyo pekee, baada ya mwaka mwajiri wake huyo alimwambia kuwa kulikuwa na ukosefu wa kibali cha kuajiri hivyo wanasikitika sana kuwa ajira yake inasitishwa. ikumbukwe kuwa kabla ya kuomba ajira hapo alikuwa na kazi nzuri na ilibidi ajiudhuru ili kujiunga na hiyo ajira mpya. sasa rafiki yangu huyo anajipanga kudai haki yake kwani anahisi ameonewa kutokana na ukweli kuwa yeye haikumpasa kujua uhalali wa kibali cha kuajiri. je wana JF hasa wanasheria kwa kesi kama hii inatakiwa aanzie wapi?
 
Nani ambaye alikuwa hana kibali cha kuajiri? Muajiri ama muajiriwa?
 
maigizo ya Bongo mpwa hayaishi, asijisumbue aaangalie mbele maaana sasa itakua wao watapeleka mwanasheria wao yeye hana mwanasheria, itakua ni usmbufu kwake, asahau aendelee mbele kikubwa apewe barua inayoonyesha hivyo kuwa walimwajiri kwa makosa then yeye aitumie barua hio kwenda huko kwenye tume ya ajira.
 

Ushauri ni mzuri japokuwa hao waliomwajiri wanasita kutoa barua ya aina hiyo nadhani kwa kuhofia kudaiwa fidia kwani huko ni kucheza na maisha ya watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…