Baada ya kuona tangazo la kazi gazetini rafiki yangu aliandika barua na kuomba kazi hiyo kama maelekezo yalivyotaka. baadaye aliitwa kwenye usaili wa kwanza akafanikiwa kupita kwani waliomba zaidi ya watu 50, waliobaki walikuwa 15 ambapo walifanyiwa usaili tena wa kujieleza ambapo rafiki yangu huyo alifanikiwa kupata nafasi hiyo pekee, baada ya mwaka mwajiri wake huyo alimwambia kuwa kulikuwa na ukosefu wa kibali cha kuajiri hivyo wanasikitika sana kuwa ajira yake inasitishwa. ikumbukwe kuwa kabla ya kuomba ajira hapo alikuwa na kazi nzuri na ilibidi ajiudhuru ili kujiunga na hiyo ajira mpya. sasa rafiki yangu huyo anajipanga kudai haki yake kwani anahisi ameonewa kutokana na ukweli kuwa yeye haikumpasa kujua uhalali wa kibali cha kuajiri. je wana JF hasa wanasheria kwa kesi kama hii inatakiwa aanzie wapi?