Naomba ushauri wa kuanzisha kampuni ya Recycling

Naomba ushauri wa kuanzisha kampuni ya Recycling

mkada

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2011
Posts
1,200
Reaction score
907
Habari wana bodi,

Mimi ni mstaafu wa umma, katika maisha yangu nimekuwa na ndoto ya kuanzisha kampuni ya kuhuisha taka chafu na kwa sasa naona nina muda wa kutosha sasa kusimamia shughuli zangu.

Naomba ushauri kwa wenye uelewa wa biashara hii ya kuhuisha taka chafu kama chupa, plastic na taka zingine.
 
Habari wana bodi....
Mimi ni mstaafu wa umma....katika maisha yangu nimekuwa na ndoto ya kuanzisha kampuni ya kuhuisha taka chafu...na kwa sasa naona nina muda wa kutosha sasa kusimamia shughuli zangu...Naomba ushauri kwa wenye uelewa wa biashara hii ya kuhuisha taka chafukama chupa, plastic na taka zingine.
MOD naomba uidelete hii uzi iliyopo jukwaa la siasa...Nilikosea kuituma kule.
 
Wazo zuri ila ingependeza ungekua umelianza kabla ya kustaafu usije maliza hela za pensheni na biashara isikulipe.

Wataalamu wanakuja wasubiri
 
Wazo zuri ila ingependeza ungekua umelianza kabla ya kustaafu usije maliza hela za pensheni na biashara isikulipe.

Wataalamu wanakuja wasubiri
Nashukuru kwa kuliona hilo...ila nimechukua tahadhari zote...na pia mimi nimekuwa nafanya biashara kwa muda mrefu sema hii ya kuanzisha kiwanda ndo nilikuwa nasubiri nistaafu
 
Nashukuru kwa kuliona hilo...ila nimechukua tahadhari zote...na pia mimi nimekuwa nafanya biashara kwa muda mrefu sema hii ya kuanzisha kiwanda ndo nilikuwa nasubiri nistaafu
Haya Mkuu kila la heri.
 
Huyu mdau anahitaji msaada kwa mwenye ujuzi lakin wakuu wanapita tu aisee.!
 
Mkuu wasiliana na sido wana machine ya kuchakata plastic
Kama sikosei bei yao ilikuwa kati ya 8-9m kutegemeana na aina ya malipo mtakayokubaliana!
 
Mkuu wasiliana na sido wana machine ya kuchakata plastic
Kama sikosei bei yao ilikuwa kati ya 8-9m kutegemeana na aina ya malipo mtakayokubaliana!
Nashukuru sana mkuu..ubarikiwe
 
Karibu i-business consult kwa ushauri, muongozo, kuandikiwa Mchanganuo, usajili na masuala yote yanayohusiana na biashara yako. Email:iconsultbuzness@gmail.com, hotline: 0659211222/0777777766
 
Back
Top Bottom