Habari wana Jf, kwanza nitangulize heshima kwenu wana jamvi.
Nimeuleta huu uzi kwenu kwasababu mpo active muda wote nina imani mtanisapoti.
Nataka kuanzisha kiwanda kidogo cha kutengeneza chakula cha kuku wa kienyeji pure, malawi, chotara n k. Yaani namaanisha breed zote za kuku wa asili.
Je ni taratibu zipi nizipitie ili niweze kufanikisha project hii? Ni lazima niwe na kampuni ili kufanya hivyo?
Ningependa project yangu niite *KIENYEJI CHICK MASHA*
Mawazo yenu jamani, nina mtaji wa milioni 6.