Naomba ushauri wa kununua gari kwa mtu alie mbali (mkoani)

Naomba ushauri wa kununua gari kwa mtu alie mbali (mkoani)

patella

Senior Member
Joined
Oct 12, 2020
Posts
114
Reaction score
325
Wakuu habari?

Kuna gari nataka kununua baada ya kuliona kwenye page ya dalali wa magari ambae yuko mwanza na gari iko mwanza, nilimpigia simu fresh tukaongea akasema inabidi nitume nusu ya hela nitakayonunua ilo gari na pia hela ya dereva ambae ataendesha iyo gari ije dar.

Sasa wakuu wenye uzoefu na kununua gari kwa mtu naomba mnijuze haya mambo huwa yananyikaje kuhakikisha sitapeliwi? ni vipi nihakiki uhalali wa iyo gari?

NB:Bado sijamtumia hela yoyote ila kesho j5 ndo nimepanga kutuma izo ela.

Sijawahi kununua gari ya mkononi kwa mtu na mbaya zaidi gari ipo mkoani.
 
NB:Bado sijamtumia hela yoyote ila kesho j5 ndo nimepanga kutuma izo ela.
  • Tafuta dereva mwenye ujuzi na magari ( awe fundi pia )
  • Mpe nauli aende kukagua gari.
Akithibitisha gari iko vyema, mtumie fedha huyu dereva uliyemtuma akamilishe biashara na arudi na gari.

Usitume fedha hata nusu, hadi gari ikaguliwe
 
Dreva anaeza fika pia akashawishiwa kuwa ukipasisha hili gari kuna laki mbili yako fasta
  • Tafuta dereva mwenye ujuzi na magari ( awe fundi pia )
  • Mpe nauli aende kukagua gari.
Akithibitisha gari iko vyema, mtumie fedha huyu dereva uliyemtuma akamilishe biashara na arudi na gari.

Usitume fedha hata nusu, hadi gari ikaguliwe
 
Tafuta dereva mwenye ujuzi na magari ( awe fundi pia )
Mpe nauli aende kukagua gari.

Akithibitisha gari iko vyema, mtumie fedha huyu dereva uliyemtuma akamilishe biashara na arudi na gari.

Usitume fedha hata nusu, hadi gari ikaguliwe

Nashukuru sana kwa ushauri
 
  • Tafuta dereva mwenye ujuzi na magari ( awe fundi pia )
  • Mpe nauli aende kukagua gari.
Akithibitisha gari iko vyema, mtumie fedha huyu dereva uliyemtuma akamilishe biashara na arudi na gari.

Usitume fedha hata nusu, hadi gari ikaguliwe
shukrani sana mkuu
 
Nilitakaga kutapeliwa laki 2 na washenzi wa Temeke wale ambao hupost magari wakiyatag kuwa yapo mikoani. Gari ilipostiwa iko Songea ila nitume advance dereva aje nalo Dar.

Katika ku reason haikuniingia akilini nikamtuma jamaa yangu alieko Dar akaongee na mwenye gari maana ilisemekana yupo Dar alisafiri kwa dharura ndio kusanukia kumbe ni chain ya matapeli.
 
Huwa naamini watu wa Dar wote ni wajanja kumbe wengine mko kama huku kwetu mkoani tu,ingekuwa mimi ningepanda Basi na fundi wangu mpk Mwanza,tungekagua gari kama tukiridhika tunafanya malipo,then tungerudi nalo Dar mdogo mdogo.
Gari za mkononi kupigwa ni dakika moja,huyo fundi ukimtuma peke yake anaweza kulishwa vihela akakudanganya kuwa gari halina shida,pia uache uvivu safari ya Dar ni siku moja tu na hizo ni hela,kwanini unataka kucheza bahati nasibu na pesa yako...?
 
Nilitakaga kutapeliwa laki 2 na washenzi wa Temeke wale ambao hupost magari wakiyatag kuwa yapo mikoani. Gari ilipostiwa iko Songea ila nitume advance dereva aje nalo Dar.

Katika ku reason haikuniingia akilini nikamtuma jaaa yangu alieko Dar akaongee na mwenye gari maana ilisemekana yupo Dar alisafiri kwa dharura ndio kusanukia kumbe ni chain ya matapeli.
daaaah [emoji23][emoji23]
 
Huwa naamini watu wa Dar wote ni wajanja kumbe wengine mko kama huku kwetu mkoani tu,ingekuwa mimi ningepanda Basi na fundi wangu mpk Mwanza ,ungekagua gari kama tukiridhika tunafanya malipo,then tungerudi nalo Dar mdogo mdogo.Gari za mkononi kupigwa ni dakika moja,huyo fundi ukimtuma peke yake anaweza kulishwa vihela akakudanganya kuwa gari halina shida,pia uache uvivu safari ya Dar ni siku moja tu na hizo ni hela kwanini unataka kucheza bahati nasibu na pesa yako...?
Tatizo muda mkuu, katika week yenye siku 7 ninapumzika siku moja tu tena saa zingine hakuna kabisa, sasa muda wa kwenda mwanza nitatoa wapi?
 
Back
Top Bottom