Naomba ushauri wa kununua kiwanja

Naomba ushauri wa kununua kiwanja

permanides

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2013
Posts
11,682
Reaction score
14,241
Wakuu nianze kwa kutoa salamu kwa wote ikiwa ni pamoja na pole kwa mihangaiko ya siku. Tukirudi kwenye kwenye kichwa cha habari, nimekiwa nikiishi kwenye nyumba za kupanga karibia miaka mitano hapa dar ila kwa sasa nafikiria nitafute kiwanja nijenge.

Wazo la kwanza nafikiria nitafute kiwanja dar cha around 10M hivi ila naona viwanja vingi vizuri ni ghali na hii M10 pengine naweza pata maeneo ya pembezoni ambayo sio mazuri sana.

Wazo la pili ni kununua kiwanja kikubwa vizuri na rahisi maeneo ya Kibaha au njia ya kwenda Bagamoyo na niwe naenda mjini asubuhi ns kurejea jioni. Maeneo ya Kibaha na njia ya Bagamoyo naweza pata kiwanja kwa 5M pekee. Niombe mtu alie na uzoefu wa viwanja / ujenzi tuweze kubadilishana uzoefu hapa.

Natanguliza shukrani.
 
Kwanza hongera kwa wazo la kujenga.

Nianze kwa kusema hivyo viwanja vizuri ghali kama unavyosema vingi vipo pempezoni mwa mji na unaweza kukipata.

Cha kwanza nikushauri kamwe usinunue na kujenga sehemu ambayo hujapapenda sababu tu kukosa pesa ya kiwanja sehemu unayoipenda(ni bora kutafuta namna nzuri kuhifadhi pesa yako uiongeze kiasi cha kutosha kuweza kununua sehemu uipendayo), hii itakusaidia kuwa comfortable na makazi yako ya kudumu.Pia maeneo ambayo unaweza kuyaona sio mazuri kwa sasa pembezoni mwa mji miaka michache ijayo inaweza ukapashangaa na usiamini jinsi patakavyokiwa pazuri(so kiwanja kiwa pembezoni mwa mji isikutishe).

mfano miaka michache iliyopita nilinunua eneo pembezoni mwa mji wakati huo wengine walikuwa wakija kupaona wanaondoka na kusema huku bado sana(kulikuwa hakuna umeme,maji ,nyumba ni chache,barabara mbovu i.e usafiri shida l...lakini sasa ni sehemu nzuri sana inayotamaniwa na wengi.

Tatu;ukiamua kununua kiwanja na kujenga nakushauri usijibana sana eneo...ni bora ukasubiri uongeze pesa ununue eneo la kujidai mambo ya kujenga pembezoni mwa mji unapata nafasi ya kujenga na parking tu kwangu mimi sio sawa.

Ukinunua eneo la kuishi wewe hakikisha unapata eneo la kujenga,parking,bustani,e.tc
 
Back
Top Bottom