Hahaha unampotosha mie niliamua kujaribu Iphone almost nina week ya 3 ni iphone 6S!
Niliagizisha ya soko la Canada! Iko freshi sana yani na ukizingatia nilikuwa natumia li Itel jamani tofauti yake na Iphone ni kama usiku na mchana! Kwanza iOS iko smooth kuliko android interms of loading apps! Natumia 1xbet kwenye android it was taking a lot of time kusubirie iload ila kwa iOS nikugusa tu kitu mwaaah! Mbali na yote natumia iOS 14 ambayo unasema hataipata na juzi wamentumia iOS 14.5 update ya GB1 sema sijaidownload bado!
Kwa support ya software pia naona iPhone wako vizuri sababu simu ya mwaka 2016 kupata support kwa miaka mitano mfululizo sio jambo dogo! Hamna android ya 2016 inayopata update ya OS current, labda utumbukize Rom za kudownload uchochoroni!
Kitu cha kiboya kuhusu Iphone ni power management tu! Aisee hii simu kabla sijatoka lazma nihakikishe iko na 100% kwanza walau ndio naweza survive nayo ila bila hivyo itazima kabla sijarudi home!
Nikiwa nafanya full matumizi naweza kuchaji mara 3 kwa siku kitu ambacho kwenye android phones kimetatuliwaga muda mrefu tu! Hawa jamaa sijajua kwenye yale ma Iphone kuanzia X na kuendelea ila haya matoleo kuanzia iPhone 8 plus kuja chini ni uongo! Battery health inasoma 100% ila simu haikai na chaji inaboa sana hasa kwa sie ambao simu hazibandukagi mikononi!