SoC by definition ni System on Chip. Kwa technology ya simu ilivyo hii SoC ndio chip inayocontain CPU ya simu, Modem ya simu (kwaajili ya network), Image signal processor au ISP (hii ndio ina fanya process zote za kuchukua picha kutoka kwenye camera na kuprocess kuwa nzuri), Graphic processing unit au GPU (hii ni kwa ajili ya vitu vyote vinavohitaji nguvu ya kuprocess graphics zake kma games na baadhi ya apps), Artificial Intelligence processors, audio and video decorder zinawezesha kuplay audio na video za format mbali mbali na zingine zina hata RAM humo humo.
Sasa hapo umeona kuwa SoC ina kuwa na vitu vyote hvyo, ikiwa weak basi na hvyo vitu vyote hapo vitakua weak.
SoC za simu zinatoka kwenye company mbali mbali lakini zinazofahamika sana ni Qualcomm, Exynos, MediaTek, Spreadtrum, Apple A series na Hisilicon
Apple A series ndio the best of the best kwenye performance ya CPU na GPU. SoC ya Apple ya mwaka husika ukilinganisha na SoC ya Qualcomm kwenye mwaka huo mara nyingi za Apple zinakuwa na CPU na GPU performance kubwa kidogo kuliko za Qualcomm.
Kwa upande wa Android Qualcomm ndio wanatengeneza SoC nzuri kuliko wote wakifatiwa na Exynos ya Samsung and Hisilicon ya Huawei. MediaTek nao wanatengeneza SoC nzuri ila sio sana na wanajulikana kwa kuwa na SoC mbaya za bei ndogo ndio unazoziona kwenye Tecno, Infinix, itel, masimu ya kichina na simu za bei rahisi kutoka kwa Xiaomi na Samsung (kma hzo A10).
Lakini pia kila company ina category mbali mabli. Low end, midrange na high end. Hizi SoC zina majina yake. Kwa mfano ukichukua simu kma Samsung Galaxy S20 zinakuwa na SoC ya Qualcomm Snapdragon 865 or Exynos 990. Hizi ni flagship SoC zenye uwezo wa hali ya juu. Lakini simu kama Samsung Galaxy A10s ina SoC ya MediaTek Helio P22 ambayo ni ndogo na haina uwezo mzuri.
Kujua SoC ya simu yako tumia app ya DevCheck au Device Info HW na angalia kundi la Hardware or SoC utaona jina la SoC ya simu yako. Pia unaweza tafta SoC ya simu online kwa kuangalia specification zake.
Ukishajua jina la SoC basi unaweza linganisha na SoC ya simu nyingine kujua zinazidiana vipi uwezo. Kwa mfano mimi simu yangu ina Snapdragon 855 nataka nilinganishe na Samsung Galaxy A51 yenye Exynos 9611. Nitaingia Google kisha nitaandika Snapdragon 855 vs Exynos 9611 kisha utachagua website ya nanoreview.net au versus.com na kusoma tofauti zake na ipi inamzidi mwenzake.
View attachment 1776875