Naomba ushauri wa tatizo langu la hedhi endelevu

Naomba ushauri wa tatizo langu la hedhi endelevu

moyochuma

Member
Joined
Oct 27, 2022
Posts
27
Reaction score
34
Hello, habari za muda huu! Wapendwa, naombeni ushauri kutoka kwa yeyote aliye na uzoefu na hali kama yangu na jinsi alivyofanikiwa kuondokana nayo. Mimi ninasumbuliwa sana na tatizo la kupata hedhi endelevu; naweza nikableed hata miezi mitatu mfululizo. Kwakweli, napitia changamoto kubwa na bado sijapata mtoto.

Juzi nilijaribu kumshirikisha ndugu yangu na akanishauri ninunue dawa ya Duphaston nitumie. Je, hii ni sahihi? Kama kuna daktari humu tafadhali naomba ushauri wako kuhusu hili.

Na kabla sijamaliza, napenda kusema kwamba niliwahi kwenda kufanya kipimo cha ultrasound mara tatu na majibu yalikuwa yanaonyesha kwamba kwenye mfuko wa uzazi kuna uchafu mwingi. Walinishauri nisafishe. Swali langu ni kwa nini kila mara imekuwa hivyo? Shida inaweza kuwa nini?

Naomba msaada wenu, asanteni.
 
Pole sana kwa hali unayopitia.

Ni ngumu sana kukusaidia kwa sababu maelezo yako hayajitoshelezi..

Kwa muktadha wa kuomba kusaidiwa kwa maelezo bila vipimo basi unapaswa kutoa taarifa zako muhimu na kwa mtiririko sahihi.

Kwanza, ueleze historia ya tatizo lako. Limekuanza lini na mpaka sasa una muda gani nalo. Unaposema hedhi ya miezi mitatu, uendeleze kwamba hukoma na kurudi baada ya muda gani. Mwezi mmoja au la!

Lakini pia, yakubidi ueleze kama ushawahi kutumia njia za uzazi wa mpango. Njia ipi na wa kwa muda gani?

Si hilo, utuambie kumbukumbu za tatizo lako. Je, hedhi yako ilikuwa sawa hapo kabla? Au ilikuwa haieleweki eleweki. Tatizo lilianzaje? Uliumwa ukatumia baadhi ya dawa na kuleta mvurugano na baadae hedhi endelevu?

Tukirudi kwenye msingi wa swali lako, kuna sababu kadhaa zinazosababisha hedhi isiyokoma au hedhi endelevu kwa maneno yako.

1. Uwiano usio sawa wa homoni.
Endapo hakutakuwa na uwiano sawa baina ya Estrogen na progesterone basi hedhi ya muda mrefu hutokea.

2. Muundo usio wa kawaida katika njia za uzazi pia husababisha hedhi isiyokoma. Hapa nazungumzia swala la Fibroids, Polyps, adenomyosis, nk.

3. Sababu nyinginezo, ikiwepo magonjwa (PID), matumizi fulani za dawa, stress, nk.

Matibabu
Ili uweze kutibiwa basi inapaswa kwanza ijulikane sababu zisababishazo tatizo.

Hivyo, yakubidi uende hospital kwa mtaalam wa magonjwa ya wanawake (Gynaecologist) akufanyie uchunguzi wa kina kabla ya kuamua kukuandikia dawa za kukusaidia.

Vipimo vitakavyofanyika ni Ultrasound, hii itasaidia kuangalia mfuko wa uzazi na kuuchunguza kuta zake na ovaries.

Pili ni Full Blood Picture (FBP) au CBC hii ni kipimo muhimu cha kujua kiwango cha damu na matatizo kama anaemia, nk

Tatu, ni kipimo cha homoni.
Hii itamsaidia mtaalam kujua kiwango cha prolactin, progesterone, Follicle stimulating hormone, nk

Sasa akishachunguza itamsaidia kujua chanzo ni nini na matibabu yake ni yepi. Kila sababu ina matibau yake tofauti..

Ushauri wa nduguyo juu ya matumizi ya Duphaston.
Kwanza, nikiri kuwa dawa hiyo hutumika katika matibabu ya tatizo hilo. Ila ni endapo tu changamoto yako inatokana na hormonal imbalance.

Sasa kuitumia bila kujua kiini haswa cha tatizo lako kunaweza kuwa unachochea tatizo zaidi.

Si hilo tu, hujui dosage yake na utaitumia kwa muda gani. Matumizi holela ya dawa ni hatari sana kwa afya yako. Epuka.

Kwa sasa, sikushauri utumie dawa yeyote ile. Mpaka pale ambapo umeshafanyiwa uchunguzi na kujulikana kiini cha changamoto yako.
 
Wanawake wengi sana wana hili tatizo siku hizi, ikiwa too much fibroid surgery ndio solution, ila kwa sababu unaonekana unataka mtoto itabidi utafute namna nyingine, ila tatizo linatibika
 
Hello, habari za muda huu! Wapendwa, naombeni ushauri kutoka kwa yeyote aliye na uzoefu na hali kama yangu na jinsi alivyofanikiwa kuondokana nayo. Mimi ninasumbuliwa sana na tatizo la kupata hedhi endelevu; naweza nikableed hata miezi mitatu mfululizo. Kwakweli, napitia changamoto kubwa na bado sijapata mtoto.

Juzi nilijaribu kumshirikisha ndugu yangu na akanishauri ninunue dawa ya Duphaston nitumie. Je, hii ni sahihi? Kama kuna daktari humu tafadhali naomba ushauri wako kuhusu hili.

Na kabla sijamaliza, napenda kusema kwamba niliwahi kwenda kufanya kipimo cha ultrasound mara tatu na majibu yalikuwa yanaonyesha kwamba kwenye mfuko wa uzazi kuna uchafu mwingi. Walinishauri nisafishe. Swali langu ni kwa nini kila mara imekuwa hivyo? Shida inaweza kuwa nini?

Naomba msaada wenu, asanteni.
Hiyo siyo hedhi ni maradhi, kamuone daktari bingwa wa magonjwa ya njia ya uzazi wa wanawake (Gyno) haraka sana.
 
You dont have PID unahitajika upate dawa kwanza zakukurudisha mzunguko wako wa kawaida kitaalamu tunaita hormonal imbalance and thats your problem anaebisha na eendelee kubisha
 
PID its very delicate issue ,inabidi apate rotation yake ya kawaida ndio tuamue PID au vp !!! You can go straight to say she got PID
 
See a specialist wa wanawake gynachologist can give you more assistance but not PID TANZANIA TUNA UROLOGIIST WACHACHE SANA
 
dadangu matatizo ya kiafya yote humalizwa na watalam a hospitali, biashara ya mitishamba utaudhuru mwili wako bure, kuna watu wamesoma miaka mingi wakijifunza huo mwili wako. Kama upo mwanza andaa fedha ya kutosha nenda mwanza hospital, hospitali hii inashughulika na mambo ya kinamama kwa asilimia 80 ya huduma zao vingine kidogo sana. Na omba a pointment ya daktari ambaye ndo mkurugenzi wa hiyo hospitali anaitwa kilonzo, kama una NHIF weka kwenye mkoba tu maana pale hapokei, ila uwe na angalau laki3 kwa kuanzia. Huyu ni super specialist wa mama na mtoto.
 
Screenshot_2024-06-30-03-08-37-149_com.android.chrome.jpg
 
Back
Top Bottom