Naomba ushauri wa tatizo langu la hedhi endelevu

Pole,yupo wakumaliza tatizo hili ndani ya wiki tu kwa miti shamba ,hakuna gharama yoyote,ila utakapo pona utatoa shukrani,unaishi mkoa gani?ikikupendeza njoo pm nikuunganishe kwa uwezo wake Mola utakaa sawa
 
Nakushauri kapime kansa tena kwa kina zaidi.
Mke wangu alikuwa na tatizo km lako na tulihangaika sana lakini dakika za mwisho tukaja gundua ana uvimbe ambao sasa ushakuwa saratani iko stage 3...
 
Pole sana, Jaribu Dawa za Himalaya Weleness





Dawa nzuri sana hii, Kesho nitakuangalizia zingine pia zinaweza weza kukusaidia.
 
Pia kuna hizi hapa kutoka India pia ila kampuni tofauti na Himalaya.



Hao ni Zest unaweza google pia ukaziona.







Hizo aina Tatu hapo pia ni nzuri sana ni za Kienyeji India, na unaweza pata maelezo yake zaidi kwenye google.
 
Mcheki huyu dr Instagram Fertility _peek
 
Tatizo la kupata hedhi endelevu linaweza kuwa na sababu nyingi, na njia bora ya kulitatua ni kwa ushauri wa kitaalam. Epuka kutumia dawa bila ushauri wa daktari na fuata maelekezo ya daktari kwa matibabu sahihi. Afya yako ni muhimu, hivyo hakikisha unapata msaada wa kitaalam kwa wakati.

Sababu Zinaweza Kusababisha Hedhi Endelevu

  1. Fibroids (Myomas):
    • Fibroids ni vivimbe vinavyotokea kwenye misuli ya mfuko wa uzazi na vinaweza kusababisha hedhi nzito na endelevu.
    • Suluhisho: Uchunguzi na matibabu yanaweza kujumuisha dawa za kupunguza ukubwa wa fibroids au upasuaji kuondoa fibroids hizo.
  2. Polyps:
    • Hizi ni vivimbe vidogo vinavyotokea kwenye ukuta wa ndani wa mfuko wa uzazi. Kama fibroids, vinaweza kusababisha hedhi nzito na endelevu.
    • Suluhisho: Matibabu yanaweza kujumuisha kuondolewa kwa polyps kwa upasuaji mdogo.
  3. Endometriosis:
    • Hali ambapo tishu zinazofanana na zile zinazopatikana kwenye ukuta wa ndani wa mfuko wa uzazi hukua nje ya mfuko wa uzazi. Hii inaweza kusababisha maumivu makali na hedhi nzito.
    • Suluhisho: Matibabu yanaweza kujumuisha dawa za kupunguza maumivu na kuzuia ukuaji wa tishu hizo, au upasuaji.
  4. Hyperplasia ya Endometrium:
    • Kuongezeka kwa unene wa ukuta wa ndani wa mfuko wa uzazi, ambayo inaweza kuwa kutokana na usawa wa homoni.
    • Suluhisho: Matibabu yanaweza kujumuisha dawa za kurekebisha homoni, kama vile progestin.
 
Point tupu Dr hujatuangusha Ushauri mzuri mno
 

Pole sana Kwanza :
OVER-BLEEDING IN NATURAL HEALTH KNOWLEDGE AND TREATMENT PLAN :

Kwa mwanamke mfumo wa uzazi upo chini ya mfumo wa INI & NYONGO / LIVER & GALLBLADDER SYSTEM ( LG )

Mfumo wa Ini Kazi zake ni kama ifuatavyo:
1. Kuzalisha maamuzi /Generate decisions
2. Kusaidia umeng’enyaji wa chakula / Helps digestions
3. Huhifadhi damu / Stores blood
4. Umeunganishwa na Tendons , kucha, macho,

5. Kwa mwanamke mfumo wa INI Hudhibiti /Control Fertility / Uzazi , Breast/ Maziwa au matiti, Ovaries , Uterus

Katika hedhi mfumo wa Ini huhusika kwa kuachia damu kwa ajili ya kuendeshea Hedhi ,
Sasa jambo hili hutegemea sana Afya ya Mfumo husika utendaji wake ( Energy Imbalance) kusababisha hormone kuvurugika

Katika Elimu asili (Heshoutang Natural Health system Knowledge) ; tatizo la over bleeding Husababishwa na energy kuwa weak / dhaifu kwenye Mfumo , hivyo kushindwa kushikilia damu kwa muda mrefu , na tatizo la Over-bleeding kutokea

Kwa maana nyingine Fire energy iko low kwenye Mfumo hivyo mfumo kuwa dhaifu ,

Tutahitaji kukufanyia diagnosis, ili kujua hali halisi ya kiafya na kutoa matibabu stahiki

Matibabu yetu ni dawa asili zenye uwezo mkubwa sana duniani , kuweza tibu kila shida ya kiafya mtu anasumbuka nayo , haijalishi ni ngumu kiasi gani , wewe tupigie na shirikiana nasi na tutakusaidia na kuondosha tatizo lako kabisa
Dawa zetu zinatoka nchini Marekani, ni elimu ya watu wa China ( Traditional Chinese medicine “ TCM “) .

Tupigie kwa namba kwenye kipeperushi chetu , usipokuwa airtel usipige , badala yake

0653048888 / 0757577995
 
Sor dr kwa kuongezea hapo,kama mtu kaweka vijiti na hedhi imekoma zaidi ya miez 6 kuna tatizo?
 
You dont have PID unahitajika upate dawa kwanza zakukurudisha mzunguko wako wa kawaida kitaalamu tunaita hormonal imbalance and thats your problem anaebisha na eendelee kubisha

Hormonal imbalance haifanyi over bleeding, hili ni tatizo kwenye viungo vya uzazi energy low mfumo unashindwa ku hold blood so inapitiliza , so anahitaji Fire energy replenishing and Circulation improvement plan ili kuvunja kama Kuna uvimbe na kuwezesha mzunguko wa damu kukaa vizuri.

Baada ya hapo ndiyo tu balance hormones, wakati mfumo upo sawa

Huwezi balance hormones kabla hujajua tatizo limetokana na nini

Hii ni advanced natural health treatment!
 
Wanawake wengi sana wana hili tatizo siku hizi, ikiwa too much fibroid surgery ndio solution, ila kwa sababu unaonekana unataka mtoto itabidi utafute namna nyingine, ila tatizo linatibika
Hizo fibroids zinarudi upya baada ya muda fulani hata kama utafanya surgery.... Kwa majority ya wanawake... Inaweza isi-apply kwa wooote 100% ila risk ya kuota upya ipo sana tuu.
 

Upo sahihi , lakini pia nao sio kila kitu wanaweza , sawa atatibiwa hata operation anaweza pona , lakini itakuwa kwa muda then same problem inaweza tokea tena , kwa sababu the toxin related can not be taken out by chemical drugs , kwa sababu kila jambo la kiafya linalotokea ni sumu / toxin , zinazotokana na Energy imbalance yaani ( Water property energy & Fire property energy)
Ili mtu aumwe ugonjwa wowote lazima hizi nishati Ziwe kwenye uwiano mbaya hivyo kuzalisha sumu mwilini na kusababisha magonjwa mbalimbali , Yanayojulikana na yasiyojulikana , yote hutoka hapo !

Na kwa sababu tunakula na kunywa , maradhi hatuwezi kwepa , lakini tunahitaji kujua kuwa tatizo hili la kiafya limeunganishwa na nishati / energy ipi ya mwili ili kutibu na kurejesha mwili kwenye utendaji sahihi ili tatizo kama lile lisitokee tena !
 
Sor dr kwa kuongezea hapo,kama mtu kaweka vijiti na hedhi imekoma zaidi ya miez 6 kuna tatizo?
Ujumbe wako sikuuona mapema.

Tukirudi kwenye mada, endapo mtu kaweka implant na hajapata hedhi kwa muda wa miezi 6 si jambo la kuogopa sana.

Labda endapo tu anahisi dalili zingine kama maumivu makali ya tumbo na mabadiliko mengine yasiyo ya kawaida.

Ila kama upo sawa, basi asijali..
 
Sina maumivu ila vaginal discharge zinabadilika sana, na pia zinaniletea hasira sana,nakua na hasira kuliko kawaida
 
Naomba kueleza kwa undani, mimi tokea ni mschana nilikua na hali ya kutopata hedhi kwa wakati, yani nilikua naweza kukaa hata miezi 5,6,7 bila kuingia hedhi....na sikua nikiumwa tumbo wala chochote kile, sema kama binti hali hii ilikua inanitesa sana....niliwahi kwenda hospital kuonana na dr akanipatia vidonge vya kupanga hedhi yani majira....nilikunywa ila hazikunisaidia kitu bas nikawa nimezoe hali ya kukaa muda mrefu bila kuingia hedhini.

Ilipofika mwaka 2013 kuna bibi alinipatia dawa za miti shamba basi nikawa napata hedhi bila shida yoyote na alinambia kua nina chango.

Kwaiyo nilikua mbaka ninywe dawa za miti shamba ndo nipate hedhi kwa wakati tofauti na hapo nilikua nakaa muda mrefu bila kuona, ilipogika 2 mwaka 2017 nina rafiki yangu aliniletea dawa nyingine tofauti ya miti shamba ilikunisaidia nipate hedhi sasa hapa ndipo nilipopata hedhi nyingi mbaka kupelekea kupoteza damu mwilini.


Baada ya hapo nilitulia kabisa sikuangaika tena kwaiyo nilikua nakaa miez 5,6,4 then naingia hedhini...sasa kufika 2020 nilitumia asali,tangawizi,na mbegu za palachichi kwaajili ya kutafuta hedhi hapa nikapata hedhi nyingi kupelekea kuishiwa damu mwilini, mbaka kupelekea kwenda kununua dawa aina ya plomotien kwaajili ya kustop ile damu....nilikaa wiki kadhaa nikawa naumwa mgongo nilienda kuchek kweny ultrsound wakanambia nina uchafu katika mfuko wa uzazi ikapelekea kusafisha kizazi kama ambavyo nilishauriwa na dr, nikawa nakaa mwezi au miez2 naapata damu kwa miez 2,3mfululizo nilipoenda kuchek wakanambia tatizo ni lilelile nikasafisha kwa mara nyingiene tena, nikakaa tena hali ikarudi tena tatizo ni lile lile nilipoenda waknambia nisafishe kwakweli sikusafisha niliondoka na sasa hali ndo hii inanitesa bado kwakweli nateseka mno...

nina picha hapa ya kipimo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…