Naomba ushauri wa vazi la harusi

Naomba ushauri wa vazi la harusi

Nyachumwi

Member
Joined
Oct 2, 2019
Posts
36
Reaction score
34
Wakuu saalam nyingi kwenu poleni na majukumu ya kulijenga taifa na familia zenu.

Kijana mwenzenu nimekata shauri ya kuwa na mke hivo nimeanza mchakato wa kufunga ndoa. Ninaomba ushauri wa rangi nzuri ya suti na viatu. Pia na maeneo ya kupata pete kwa bei ambayo ni affordable.

NB. Mimi kwa kuanzia nimependekeza hizi hapa mbili za kuanzia.

Mimi ni mweusi japo sio kama msudani kusini.

Screenshot_2020-07-21-11-19-53-1.jpeg
 
Tembelea maduka ya suti za harusi uchague ukipendacho wewe kulingana na mfuko wako, umbile lako, rangi yako na matakwa yako! Tusichoshane humu mweeh
 
Tembelea maduka ya suti za harusi uchague ukipendacho wewe kulingana na mfuko wako, umbile lako, rangi yako na matakwa yako! Tusichoshane humu mweeh
Maduka yapo wapi mkuu usichoke
 
Maduka yapo wapi mkuu usichoke

Ndugu yangu, Kariakoo kuna maduka ya suti za harusi. Kuna duka linaitwa Kwamringi nafikiri ni mtaa wa Aggrey karibu na bank moja. Ukiwa Kariakoo ukiulizia kuna maduka mengine mengi tu. Sinza pia kuna maduka ya suti za harusi ila bei zao ziko juu ingawa nguo zao nyingi zinafanana na zile za Kariakoo! Wahi mapema zunguka kariakoo utafanikiwa!
 
Bwana harusi wa mwendokasi, nenda kwa jm international mbobezi wa suti, bei zake ni laki 7
 
Asante mkuu
Ndugu yangu, Kariakoo kuna maduka ya suti za harusi. Kuna duka linaitwa Kwamringi nafikiri ni mtaa wa Aggrey karibu na bank moja. Ukiwa Kariakoo ukiulizia kuna maduka mengine mengi tu. Sinza pia kuna maduka ya suti za harusi ila bei zao ziko juu ingawa nguo zao nyingi zinafanana na zile za Kariakoo! Wahi mapema zunguka kariakoo utafanikiwa!
 
Nakushauri kama hutajaili ushone mwenyewe tafuta fundi mzuri akutolee kitu kinakufiti kabisa
 
Back
Top Bottom