Naomba ushauri: Wapi nipate msaada wa mtaji juu ya mradi wangu wa matikiti maji, no 0757494890

Naomba ushauri: Wapi nipate msaada wa mtaji juu ya mradi wangu wa matikiti maji, no 0757494890

Kaka ee nipe mchanganuo halisi na ekari ngapi zitatosha halafu kwa muda gani matikiti yatakaa shamba na wapi soko lilipo sio unalima wakati soko hauna ili tuanze kazi hii...
 
Labda lkn usiwe na ndoto kubwa kwani kikija kiasi kidogo watu wanatoana macho!
PM ME KAMA MCHSNGANUo(PLAN) YAKO IKO VYEMA...
 
Nina shamba kubwa sana&mitaji ipo ila sina ufahamu wa agriculture_agrobusiness ss tunaweza kufahamishana &tukaweza kuanza kazi kwani ajira hamna labda tukajitosa ili kuwaelekeza wenzetu kuliko kulalamika wkt vyeti vipo ktk sanduku..
 
Huu mchanganuo hauko sahihi,profit ya M.196 toka M.8 tu toka kwenye heka 4,yan inazidi hata vitunguu ambavyo ndio vinaongoza kwa faida.
 
Kulima kwetu sio ishuu mbona nilianza kulima nikiwa na umri wa miaka 12...
Nipe dili hilo ww changanua vizuri ama nitupie no ya sm ktk PM...
 
Ndugu yangu kama garama zingekuwa kubwa hivi wakulima wasingekuwepo huu mchanfanuo umeufanya kishule shule zaidi na sio kuhalisia .
Kiuhalisia garama ya eka 2 ni laki sita tu hadi unavuna.ukiondoa garama za usafirishaji hadi sokoni kwani unaweza kuuzuia shambani.
Mimi nimelima eka 1 Ruvu nimetumia laki 3 ila ya mvua za masika

Mkuu unaonekana una uzoefu wa kilimo cha matikiti Ruvu. Mimi nataka niingie kwenye kilimo hicho. Je naweza kupata shamba la kukodi la eka moja kwa kilimo hicho hapo Ruvu? Gharama ya kukodi shamba inaweza kuwa sh ngapi kwa muda gani? Soko lake na usimamizi vimekaaje? Je naweza kupata vibarua na msimamizi mwaminifu huko hadi wakati wa mavuno bila shida? Mimi nategemea kuwa na nafasi ya kwenda shambani siku za J1, J2 na sikukuu. Ninapendelea kuuzia huko huko shambani baada ya mavuno. Je naweza tumia kiasi gani cha pesa hadi mavuno na mapato yamekaaje baada ya mauzo shambani kwa eka moja?
 
Back
Top Bottom