Naomba ushauri waungwana

Naomba ushauri waungwana

R Mbuna

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
2,283
Reaction score
5,371
Habari za wakati huu wanajamvi,

Kutokana na kasi ya muheshimiwa mkuu wa nchi sasa naona mji wa Dar haunifai tena nataka kwenda kujishughurisha rasmi kwenye kilimo moja kwa moja.

Sasa nina mashamba yangu huko Kilombero na kilimo ninachitegemea kwenda kufanya kule ni cha mpunga na mahindi ingawa hapo mwanzo tulikuwa tunalima na wife ndiye anayesimami ila sijayaona mafanikio kama yele niliyokuwa nikiyatarajia.

Ushauri ninaouhitaji ni kujua aina ya mbegu nzuri ya mpunga ambayo nikilima nitapata magunia mengi na mchele wake unakuwa mzuri pia na mahindi mbegu ipi ni nzuri na inapatikana kwa mwakala gani wa pembejeo za kilimo?

Nitashukuru sana kama nitapata ushirikiano wenu wanajamvi maana kazi za kuongeza sifuri sasa hivi haziwezekani tena ukijisahau tu unatumbuliwa so sihitaji pressure za kukosa kazi bila ya kujiandaa.
 
Back
Top Bottom