Naomba ushauri wenu, nina TSh milioni 1.5, ni biashara gani naweza kuanzisha kwa kiasi hiki?

Naomba ushauri wenu, nina TSh milioni 1.5, ni biashara gani naweza kuanzisha kwa kiasi hiki?

Dadakidoti

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2024
Posts
399
Reaction score
1,409
Bila shaka familia ya JF, wote mko salama.

Nisiwachoshe, naomba niende moja kwa moja kwenye mada. Mimi ni miongoni mwa wale wa "pangu pakavu," lakini namshukuru Mungu kwa kunijalia uhai na afya njema.

Najua humu ndani wengi wenu ni wenye vipato vikubwa, lakini naomba msisahau kuwa hata sisi walala store bado tumo. Kama ilivyo katika safari ya mamba, hata kenge wapo, hivyo msitubague.

Nije kwenye hoja: kwa kazi yangu hii yenye mshahara mdogo, nimejinyima sana na kufanikiwa kuweka akiba ya shilingi milioni 1.5. Naomba ushauri wenu, ni biashara gani naweza kuanzisha kwa kiasi hiki?

Tafadhali nisaidieni, jamani.
Muwe na siku njema!
 
Bila shaka familia ya JF wote mko salama.
Nisiwacho niende moja kwa moja kwenye mada. Mwenzenu mimi ni wale wa pangu pakavu. ila namshukuru Mungu kunijalia uhai na afya njema.
Humu mlio wengi najua ni wale wenye vipato vikubwa ila msisahau hata sisi walala store bado tumo. make katika safari ya mamba na kenge wapo hivyo msitubague.
Nije kwenye point mdada kwa kazi yangu hii ya mshahara nimejinyima na nimefanikiwa kumake 1.5 m. je naweza anzisha biashara gani.
msaada wenu jamani.
Muwe na siku njema
Uko mkoa gani mrembo wangu ?
Lakini Mimi nataka na kuoa binti anayejielewa Kama wewe ,vipi hatuwezi kuwa wapenzi Sasa ?
 
Tembelea masokoni utapata idea mkuu, au kama una rafiki anafanya ishu zake soko lolote mtembelee upige nae sofa mbili tatu. Umuulize kijanja kama unaweza fremu maeneo hayo.

Juice zinatembea sana masokoni, mambo ya miamala ya kifedha, vinywaji baridi/vikali vya bei chee, vifungashio na mifuko nk
 
asante sana nitalifanyia kazi
 
1.5m

ebu endelea kujinyima tena walau ifike 3m

Kama huwez basi uza nafaka upate hzo mia mbili mbili kwa siku huwez kosa 5000

Mchele kg 200
Maharage kg 200
Sukari kg 50
Ngano kg 25
Chumvi
Viazi gunia 1
Vitunguu gunia 1
Viungo vya pilau na chai
Mahindi yalikobolewa kg 50
Navingine vingi kama hvyo
 
Back
Top Bottom