mtanzania in exile
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 1,379
- 1,276
Katika mwaka mmoja tu (june 2011 hadi July 2012) wake za watu watatu wamenifata kunitaka kimapenzi. Ninachotaka kujua ni kwa nini? ni kosa gani nifanyalo kiasi kuwa wake za watu wafikiri nawataka?
Wote nimewakwepa, lakini kinachonishangaza ni kwa nini hasa waache waume zao na kunifuata mimi? Wakati huo huo kuna mwanamke ambae yuko single na ananivutia mno lakini ananipiga chenga mwaka na nusu sasa na anasingizia eti ananihisi mimi ni player, jambo ambalo sio kweli kabisa!
Mmoja kati ya hawa wake za watu amefika hadi kudai kuwa anajua hasa kuwa ninamzimia, na ni woga tu ndio unaonizuia mimi kumfuata, na kwa sababu hiyo ndiyo yeye kaamua ku make the first move. Wote wamedai kuwa ucheshi wangu na tabasamu zangu niwaonapo njiani na sehemu za mikusanyiko ni ishara ya kuwa niko interested. Hilo sio kweli kwani hiyo ni hulka yangu kuwa mcheshi kwa kila nimjuae sio kwao wao tu, tabasamu kwangu ni jambo la kawaida. Daima huwa na dakika chache za kusimama kusalimiana na kuzungumza na niwajuao nikutanapo pahali popote pale.
Hivi ndugu zangu kuwa mcheshi na mchangamfu ni kosa? Huku ugenini ukianza kutokusalimia au kutotaka kujuana na watanzania wenzako ni hatari, kwani mbali ya wao kukuona kuwa unajipenda na kuwadharau wenzako pia nao watakutenga, jambo amablo sio jema hasa ukizingatia kuwa tuko mbali na familia zetu, binaadam mzima leo hujui kesho utaamkaje.
Hebu niambieni nifanyaje ili kuepukana na matatizo haya. Imeanza wake wa watu kuhisi nawataka, isije ikaja kufika waume zao kufikiria nawaibia wake zao.