ahsante kwa ushauri wako ndugu, lakini napenda nikukosowe kidogo kuhusu hapo uliposema kuwa watu huku nje tunatanuwa sana. Hilo sio kweli na ni mawazo ya wengi wa waliopo nyumbani. Ukweli hutokea baadhi ya siku kukawepo na mikusanyiko ya hapa na pale na sio kila mwisho wa week end, mara nyingi hukuntana kwa sababu kuna jambo iwe harusi, msiba n.k hivyo ndivyo ilivyo pande hizi niliko, sijui kwengine though
Usinilaumu kufikiria hayo hasa kwa tunavyosikia jinsi maisha ya huko yalivyo. Tunasikia huko hakuna wakati wa kupoteza kwa ajili ya kazi. Sasa unapotwambia kuwa wake watatu wa watu tayari wanakufuatilia bila shaka ipo nafasi ya kujitanua. Halafu haya mawakati unayokutana kutana na wenzako kiasi cha wanamama kukushobokea yanapatikana wapi, iwapo hakuna mataimu ya kutanua huko?