Kaka pole sana kwa yaliyokukuta, before I jump to the conclusion; huyu dada alikuzungusha sana nafikiri ile ilikuwa ni sign ya kukwambia kwamba ana mwingine hakuwa radhi kumwacha. "Unajua jamani wanawake na wanaume" naomba tujifunze kusoma alama za nyakati kwa wale tunaowahitaji, tulionao tayari au tunaotegemea kuwatafuta. Lazima uwe na msimamo wa maisha yako kwenye mapenzi na yule unayetegemea kumpenda.
Tusiwe ving'ang'nizi pasipo sababu. Kaka sitaki kujua umri wako, naomba kuanzia sasa ukue na uwe na uelewa wa mtu wa NDIYO au HAPANA. Haina sababu ya kukupa moyo hapa eti uvumilie utakuwa unatenda dhambi which end of he day utahukumiwa wewe. Imagine mtu kakwambia ana bwana yake wewe unaanza kulazimishia penzi huoni wewe unakasoro au unataka mwenzio atende dhambi ambayo hakutarajia kuifanya.
Mimi ni mwanamke ila tuna kasoro moja, penye ndiyo huwa tunaweka hapana, na penye uongo ndiyo tunakaa kwa muda mrefu tukisubiri miujiza itendeke. Huyo dada hana tofauti na kina ABLAKADABLA au kwa lugha nyingine MWANA MAZINGAOMBWE. Acha kutojiamini na kukata tamaa. Acha kujiona wewe una mikosi ni mambo ya kizamani kwanza siamini kwamba kuna mikosi. Unakuwa umekutana na wrong number. SOMA ALAMA ZA NYAKATI na wanawake unaokutana nao, na wapi UMEKUTANA NAO. Usitegemee product ya kike ya BAA, DISCO, au kwenye DALA DALA umekula wa chuya. Kaa tulia, jenga KUJIAMINI.
Pole na CHAPA MWENDO, Mungu anakuepusha na mambo mengi.